-->

WATU 15 WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE 85 KUJERUHIWA NCHINI MISRI

http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/28f8a22292295b1ea9b96128c16467ce_XL.jpgWatu wasiopungua 15 wameuawa katika machafuko yaliyotokea leo nchini Misri katika maadhimisho ya mwaka wa 40 wa tangu yalipoanza mashambulizi ya Misri dhidi ya vikosi vya utawala wa Kizayuni wa Israel katika vita vya mwaka 1973.
Khaled al Khatib, mmoja wa maafisa wa Wizara ya Afya ya Misri amethibitisha habari hiyo. Saba kati ya watu hao wameuawa katika Medani ya Ramses mjini Cairo. Watu wengine 85 wamejeruhiwa katika machafuko yaliyotokea kwenye maeneo tofauti ya Misri.
Polisi wamewafyatulia risasi na mabomu ya kutoa machozi makundi ya watu waliokuwa wanaandamana huku wengine wakijaribu kuingia kwenye Medani ya Tahrir ambako maelfu ya watu wanaounga mkono jeshi la Misri walikuwa wamekusanyika kuadhimisha siku hiyo.
Huko Delga, kusini mwa Cairo, duru za hospitali zimeliambia shirika la habari la Reuters kwamba polisi walifyatua risasi hai katikati ya kundi la watu waliokuwa wanarusha mawe, na kumuua mtu mmoja.
Watu wengine wameuliwa katika maeneo mengine yaliyoshuhudia machafuko nchini Misri.
source:irani swahili radio
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment