-->

PAMOJA NA KULIPA FAINI, TFF WAMUONDOA SHAFFIH DAUDA KWENYE UCHAGUZI WA TFF

PICHA ZA GWIJI WA UCHAMBUZI WA MPIARA NCHINI TANZANIA SHAFFIH DAUDA KATIKA HARAKATI MBALI MBALI ZA KISOKA KITAIFA NA KIMATAIFA

Pamoja na uzoefu mkubwa alionao katika soka lakini bado ametupwa nje tena kwenye uchaguzi wa TFF baada ya kuondolewa kwenye uchaguzi uliopita kwa kukosekana kwa moja ya karatasi za fomu yake ya maombi,kitu ambacho ilihisiwa kuchanwa kwa makusudi ikiwa kama fitna ya kumuondoa Shaffih Dauda na sasa wamemuondoa kwa kuonekana kuwa ni mtu asiye na uzoefu kwani taarifa zake za kiuongozi katika klabu ya Bom bom fc haionyeshi kuwa na uzoefu wa miaka mitano.Kigezo kingine kilichotumika kumuondoa kwenye uchaguzi ni kile cha madai ya kutolipa faini aliyoagizwa kulipa kitu ambacho si kweli soma pos hii KUHUSU KULIPA FAINI YA SHAFFIH DAUDA 
Hii hapa chini ni nukuu ya post ya Shaffih Dauda akieleza kuhusu kuondolewa kwake kwenye uchaguzi wa TFF"Breaking News ! Kamati ya Uchaguzi ya TFF imekata tena jina langu,safari hii wanasema walishanitoa kwa kukosa uzoefu na sikukata rufaa,SWALI: LINI NA WAPI HIYO SABABU YA KUKOSA UZOEFU WALIWAHI KUNITAARIFU?,sababu pekee ninayoifahamu iliyotolewa na kamati ya uchaguzi ilikuwa ni ukosefu wa maadili na wakanipeleka kwenye kamati za maadili. KWELI SIMBA AKIZIDIWA ANAKULA HADI MAJANI..."
Kaa nasi Daima ili kujua taarifa mbali mbali
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment