Mario Balotelli
GWIJI wa soka
duniani, Diego Maradona amesema kwamba Mario Balotelli ni mwanasoka
nambari nne kwa ubora hivi sasa duniani baada ya Messi, Ronaldo na
Neymar.Katika kipindi cha maswali na majibu mjini Milan, gwiji huyo wa
Argentina alielezea mapenzi yake kwa nyota huo wa zamani wa Manchester
City na kwamba walianza kufahamiana vyema na mshambuliaji huyo wa Italia
alipomtumia picha anavuta cigar ya Cuba.
Namba 10
huyo wa zamani, mmoja wa wanasoka bora kabisa kuwahi kutokea duniani
alisema: "Mawasiliano yangu ya kwanza na Mario ni pale aliponitumia
picha yake anavuta Cuban. Naipenda! Nilicheza,"
Maradona
pia anataka kukutana na Balotelli ili ampe ushauri nasaha mshambuliaji
huyo wa AC Milan."[Watu lazima] wamuache na amani. Ningependa kuzungumza
na Mario peke yetu, katika chumba chetu, na kumfafanulia uzoefu mbaya
wote niliopitia.'
Pamoja na
hayo, licha ya kuwa shabiki mkubwa wa Balotelli, Maradona anampa nafasi
ya nne mshambuiaji huyo wa Milan katika orodha yake ya wachezaji bora
duniani, akimuweka nyuma ya Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Neymar.
Wakati
huo huo, nyota huyo wa zamani wa Napoli amesema kwamba anapenda kurudi
katika klabu hiyo kama kocha mara kocha wa sasa, Rafa Benitez
atakapoondoka.
Akiwa
ameshinda mataji mawili ya Serie A na timu hiyo miaka ya 1987 na 1990,
Nyota huyo wa Amerika Kusini amesema: "Wakati (Rafa) Benitez
atakapoondoka ningependa kuikochi Napoli,".
Pamoja na
hayo, mtu mzima huyo mwenye umri wa miaka 52 si rahisi sana kwake
kupata nafasi hiyo: "Kuna mabadiliko ya makocha yanafanyika kila sehemu
kutoka Hispania hadi Italy hadi England hadi Urusi, lakini watu fulani
wananiogopa mimi. Ndiyo maana sikochi,."Maradona aliifundisha Argentina
hadi kuifikisha Robo Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010 na kisha
akaenda Dubai kufundisha klabu ya Al Wasl kwa msimu mmoja
Blogger Comment
Facebook Comment