mefahamika
kwamba bara la Afrika lina
mabilionea wengi sasa hivi kuliko ilivyokua
ikifikiriwa ambapo hii imefahamika baada ya jarida la Ventures kuripoti kuwa pamoja na idadi ya mabilionea kuzidi kuongezeka bado
asilimia kubwa ya Waafrika ni
masikini wa kutupwa.
Kabla ya hii ripoti, idadi ya mabilionea wa Afrika
ilikuwa 16 lakini imeongezeka na kufikia 55 na jarida hili limeweza kuwagundua
mabilionea wengi kwa kuchunguza kwa siri ili kuepuka baadhi yao ambao ambao
wanaficha taarifa za utajiri wao, yani huwa hawapendi kuzitoa kwa wanahabari.
kati
ya mabilionea hao 55, 20 wanatokea Nigeria
na wanajumuisha wafanyabiashara wa mafuta huku Afrika kusini na Misri
zikiwa na mabilionea tisa ambapo
alietajwa kuwa ni tajiri kuliko wote Afrika ni Mnigeria Dangote ambae ana utajiri wa dola bilioni 20.2
Dangote
alitengeneza utajiri wake kupitia biashara ya saruji na hadi leo anaongoza
kampuni ambayo inahusika na biashara za unga wa kupikia, sukari pamoja na mafuta.
Mwanamke
tajiri kuliko wote Afrika
anatokea Nigeria pia ambaye Folorunsho Alakija ambae kampuni yake ya fama oil inamilki visima vya mafuta
ambavyo alivipata mwaka 1993, alianza
kama mwanafunzi wa masuala ya mitindo huko London na alikuwa akibuni mavazi ya rais wa zamani wa Nigeria Ibrahim Babangida.
Tajiri toka afrika kusini Nicky Oppenheimer ana utajiri wa
dola bilioni 6.5 utajiri ambao ulipatikana kwenye madini hususan madini ya
almasi ambayo amerithi toka kwa familia yake.
Pamoja na hii ripoti kunifikia bado haijanipa
mabilionea wengine waliobaki wanatoka nchi gani.
Blogger Comment
Facebook Comment