Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Joseph Konyo amethibitisha tukio hilo na kwamba mkono huo uliokuwa umewekwa kwenye begi ukiwa umefungwa kwenye mfuko mweusi wa plasitiki na kuviringishwa kwenye karatasi nyeupe ya nailoni, umekutwa ukiwa mbichi.
Konyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Mwanza (RCO), alieleza kuwa watuhumiwa hao (majina yanahifadhiwa) wenye umri wa miaka 36 na 43 (ni waganga wa jadi wawili) na mfanyabiashara ana miaka 48.
Taarifa zilizotolewa katika jeshi hilo na kuweka mtego huo kisha makubaliano ya kununua viungo hivyo kutoka kwa watuhumiwa hao (wauzaji), walimhakikishia mnunuzi (polisi) kuwa wanaweza kupata kichwa, mikono, miguu na sehemu za siri za binaadamu endapo mteja angehitaji.
kwa mujibu wa makubaliano hayo wauzaji hao ambao ni Waganga walitaka kupewa shilingi milioni 100 kwa mkono huo mmoja lakini baada ya kufanya mazungumzo ya kibiashara na wao kuona kitita cha fedha, walilegeza bei na kujikuta wakitiwa mbaroni
0 comments :
Post a Comment