-->

MPASUKO MKUBWA WAJITOKEZA KWA WANACHAADEMA,NYARAKA ZA CHAMA ZAWEKWA MTANDAONI

Kwa siku za karibuni, umezuka mjadala
 mkali ndani ya mtandao huu pendwa
hasa baada ya Samson Mwigamba
ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA
Mkoa wa Arusha kuwatuhumu viongozi
wa kitaifa wa CHADEMA kuwa
wamebadilisha katiba kinyemela kwa
kuondoa ukomo wa uongozi wa awamu
mbili ili waendelee kubaki madarakani.
Mwigamba ametoa shutuma hizo
akitumia jina bandia la Maskini
Mkulima. Katika shutuma zake
Mwigamba amesema yafuatayo;
Wakati tukifanya mabadiliko ya katiba
mwaka 2006 hatukugusa kipengele
kinachomzuia kiongozi kuongoza
kwenye nafasi moja kwa zaidi ya
vipindi viwili vya miaka mitanomitano.
Lakini wakati katiba inachapwa chini ya
uongozi uliopo, kipengele hicho
kiliondolewa kinyemela. Mambo
yanayotokea hivi leo yanaonyesha
dhahiri kipengele hicho kiliondolewa
kwa makusudi kwa maslahi na kwa
faida ya viongozi waliopo madarakani
kwa sasa. Hiki kinaweza kuchukuliwa
kama kitendo kidogo lakini kama
viongozi wetu wanaweza kutokuwa
waaminifu katika jambo kama hili, ni
dhahiri hawawezi kuaminika na
wanaweza kufanya mambo mengine
makubwa nayenye athari
zisizomithirika kwa chama.
Ni muhimu wanachadema mkafahamu
kwamba kitendo cha kuondolewa kwa
kipengele hicho ndicho kinacholeta
mpasuko leo kwenye chama
unaotokana na Mbowe na Zitto
kupigania uenyekiti. Kama
kingekuwepoleo Mbowe alikuwa
anakatazwa na katiba kugombea
kipindi cha tatu na hivyo vita iliyopo
kati yake na Zitto isingekuwepo na
chama kingekuwa imara zaidi. Ni
dhahiri Mbowe aliondoa kipengele
hicho kwa makusudi ili aweze
kuendelea kugombea bila mwisho na
huu ni udikteta kama ule tu wa akina
Lyatonga Mrema, John Cheyo na
wengineo, na wanachadema hatupaswi
kuuruhusu si kwa Mbowe tu bali kwa
yeyote atakayepata nafasi ya kuwa
mwenyekiti wa chama chetu.
Mara baada ya taarifa hiyo ambayo
ilibebwa kwa jina la Wito kwa wana
CHADEMA wote! ambayo ilieleza
madhaifu ya chama na kubadilishwa
kwa vipengele vya katiba kinyemela,
Dr Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA
alitoa ufafanuzi ufuatao;
WanaJF,
Nataka kuwahakikishia wanachadema
wote, kuwa nilikuwepo nimekuwa
ndani ya Chadema kuanzia 1998
ambapo nilikuwa Makamu Mwenyekiti
Bara, na baadaye 2003 Kaimu Katibu
Mkuu, na hatimaye Katibu Mkuu. Hivyo
nimeshiriki kikamilifu kuandaa Katiba
ya 2004 na pia Katiba ya 2006 baada
ya Rebranding ya Chama. Nataka
niwahakikishie wanachadema, hakuna
toleo lolote la Katiba ndani ya Chadema
imeweka " muda wa Uongozi kuwa
vipindi viwili tu", kuanzia Katiba
aliyoiasisi Mzee Mtei na kupitishwa na
Mkutano Mkuu, wala si ya 2004 au ya
2006. Kama kuna mtu anasema
ilikuwepo na imeondolewa kinyemela,
basi aonyeshe kifungu hicho kwenye
Katiba yeyote ile, au miniti za kikao
chochote kile.
Hata hivyo, majibu hayo ya Dr Slaa
yanaonekana kutofautiana na yale ya
JOHN MNYIKA aliposema kuwa
kwenye katiba ya 2004 kipengele cha
ukomo wa uongozi kiliwekwa lakini
hakikuingizwa kwenye katiba ya 2006.
John Mnyika anasema;
Kuhusu Katiba, nina nakala mango
(hard copy) tu ya katiba ya 2004,
ilikuwa na kipengele cha vipindi viwili
vya nafasi ile ile. Hata hivyo, katiba
mpya iliyoandikwa mwaka 2006
haikuwa na kipengele hicho. Hivyo, sio
kwamba kimeondolewa kinyemela ila
hakikuwepo kwenye katiba mpya. JJ
Baada ya malumbano hayo, nilifanya
utafiti mdogo ili kujiridhisha na hoja
zilizotolewa na viongozi hao. kwa
msaada mkubwa kutoka kwa wadau
muhimu ndani ya CHADEMA,
nimefanikiwa kupata nyaraka zifuatazo
1. Nakala ya Katiba ya CHADEMA
ya mwaka 2004 iliyoandikwa
kwa lugha ya Kiingereza
2. Nakala ya Katiba ya CHADEMA
ya mwaka 2006 iliyoandikwa
kwa lugha ya kiswahili
3. Muhtasari wa Mkutano Mkuu
Maalum wa CHADEMA
uliofanyika katika ukumbi wa
PTA Dar es Salaam tarehe 13,
Agosti 2006
Nitajaribu kuweka vipengele muhimu
mahsusi kwa mjadala huu. Nitajikita
kwenye hoja moja tu ya Mwigamba
kuwa Viongozi wamefanya
marekebisho ya katiba kinyemela kwa
kuondoa ukomo wa madaraka ili
waendelee kuwepo madarakani.
Katiba ya mwaka 2004 ipo wazi kabisa
katika hoja ya ukomo wa madaraka.
Ibara ya 6.3.2 kipengele cha (c)
kinasema ifuatavyo; ''Leaders who
finish their term of office can be
eligible for re-election provided he
qualifies but no leader can hold the
same post at the same level of the
party structure for more than two
terms. Kutokana na kipengele hiki,
kauli ya Dr Slaa kuwa hakuna katiba ya
CHADEMA iliyoweka ukomo wa
madaraka ni ya kushangaza
ikizingatiwa kuwa yeye ni Katibu Mkuu
na hakupaswa kusema uongo mbele ya
watu ambao wanaelewa mengi kuhusu
katiba hizo.
Katika Mkutano Mkuu Maalum wa
mwaka 2006 ambao ulikuwa na ajenda
4 ambazo ni;
1. Kufungua Mkutano
2. Maboresho ya Katiba
3. Maazimio juu ya Katiba Mpya na
4. Kufunga Kikao
ulijadili vifungu 10 ambavyo
vimefanyiwa marekebisho kutoka
kwenye katiba ya 2004. Kati ya
vipengele hivyo, kipengele cha ukomo
wa madaraka hakimo na hii ni kusema
kuwa hoja hiyo haikuwa na
marekebisho. Vipengele vilivyofanyiwa
marekebisho kwa mujibu wa muhtasari
huo vimeambatishwa na taarifa hii.
Katiba ya Mwaka 2006 ndiyo
inayolalamikiwa kuchakachuliwa kwa
vile kipengele cha ukomo wa
madaraka hakimo na hakuna mkutano
uliojadili hoja hiyo. Kutokana na hali
hiyo, ni wazi kuwa hoja za Samson
Mwigamba ni sahihi na viongozi wa
CHADEMA hususan DR WILBROAD
SLAA NA JOHN MNYIKA wametoa
majibu ya uongo kupinga hoja za kweli.
kwa mantiki hiyo, ni wazi kuwa katiba
imechakachuliwa kwa maslahi ya
wanaotetea uchakachuaji huo.
Nawasilisha.
Attachment 118833Attachment
118834Attachment 118835Attachment
118836Attachment 118837Attachment
118838Attachment 118839
KATIBA YA MWAKA 2006
6.3 Uchaguzi wa Viongozi na Muda wa
Uongozi
6.3.1
Utaratibu wa Uchaguzi
(a) Uchaguzi wa viongozi utazingatia
taratibu na sifa za uongozi kama
zilivyofafanuliwa katika kanuni za
Chama.
(b) Maombi ya uongozi yatafanywa
kwa maandishi kwa kujaza fomu
maalum
zilizoidhinishwa na Baraza Kuu la
Chama.
(c) Majina ya wagombea wote wenye
sifa zilizotakiwa yatapigiwa kura za siri
na kikao
kinachohusika na mshindi atapatikana
kwa uwingi wa kura usiopungua 50%
ya
wapiga kura halali waliohudhuria kikao
cha uchaguzi.
(d) Uchaguzi wa viongozi wa
Mabaraza ya Vijana, Wanawake na
Wazee utafanyika
kwa kuzingatia Ibara hii ya Katiba.
(e) Ikiwa katika chaguzi za chama kura
za wagombea zinalingana Mwenyekiti
atakuwa
na kura ya turufu.
6.3.2 Muda wa Uongozi
(a) Kila uongozi uliochaguliwa au
kuteuliwa wakati wa uchaguzi mkuu
wa Chama
utashika wadhifa wake kwa kipindi cha
miaka mitano.
(b) Kiongozi aliyechaguliwa au
kuteuliwa baada ya uchaguzi mkuu
atashika wadhifa
wake hadi kipindi cha uchaguzi mkuu
kinachofuata.
(c) Kiongozi aliyemaliza muda wa
uongozi ana haki ya kugombea na
kuchaguliwa tena
mradi awe anatimiza masharti ya
kuchaguliwa kuwa kiongozi.
(d) Muda wa uongozi unaweza
kufupishwa kama mamlaka iliyochagua
au kuteua
itaamua hivyo.
(e) Ibara hii itahusu pia viongozi wa
Mabaraza ya Vijana, Wanawake na
Wazee wa
CHADEMA.
6.3.3 Kurekebisha tarehe ya Uchaguzi
Mkuu wa Chama
(a) Tarehe ya uchaguzi mkuu wa
Chama inaweza kurekebishwa kwa
kusogezwa mbele
kwa muda usiozidi mwaka mmoja toka
mwisho wa uhalali wa uongozi uliopo.
(b) Mamlaka ya kufanya marekebisho
haya yameachiwa Kamati Kuu
(c) Kamati Kuu ndiyo itapanga tarehe
ya uchaguzi wa Mabaraza ya Vijana,
Wanawake
na Wazee wa Chama.
6.3.4 Kukoma kwa Uongozi
(a) Kwa kiongozi kujiuzulu kwa hiari
yake
(b) Kwa kiongozi kuachishwa uongozi
au kufukuzwa uanachama
(c) Kwa kiongozi kushindwa kutimiza
wajibu wake kwa mujibu wa masharti
ya
katiba, kanuni au maadili ya Chama.
(d) Kwa kufariki
(e) Ibara hii inahusu pia uongozi wa
Mabaraza ya Vijana, Wanawake na
Wazee ya
Chama

SOURCE:JAMII FORUM
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment