-->

MGANGA WA KIENYEJI ANUSURIKA KUUAWA BAADA YA KUSHINDWA KUMFUFUA MTU ALIYEKUFA

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la HAMISA BENJAMINI mwenye umri wa miaka 26 mkazi wa kijiji cha Katoro wilayani Geita ambaye ni mganga wa kienyeji amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira baada ya kushindwa kumfufua marehemu MBELWA LUKAZA.
 
Tukio hilo limetokea siku chache baada ya jeshi la polisi mkoani Geita kwa kushilikana na wataalamu kutoka ofisi ya mkemia mkuu kanda ya ziwa kufukua kaburi linalosadikiwa kuwa na viungo vya mtoto SHABAN MAURID mwenye umri wa miaka 15 aliyefariki dunia miaka mitatu iliyopita na kuonekana akiwa hai.

Akielezea chanzo cha sakata hilo mke wa marehemu TAUSI EMMANUEL amesema kufuatia kifo cha ghafla cha mumewe MBELWA LUKAZA kilichotokana na ajali ya gari Agosti 28 mwaka huu aliamua kwenda kwa mganga huyo wa kienyeji ambaye alimuhakikishia kuwa mumewe hajafa na kuwa anao uwezo wa kumrudisha.

Baada ya kushindwa kufufuliwa kwa marehemu huyo ndugu na marafiki zake walimtaka mganga awarejeshee gharama walizomlipa zilizokadiriwa kuwa zaidi ya shilingi milioni tano kama ilivyoelezwa na HUSSEIN NASSOR.
 
Kwa upande wake Mganga HAMISA amekiri kuahidi kumfufua marehemu huyo ambaye kwa sasa amedai kuwa ametoroka kutokana na kelele na vurugu zilizofanywa na ndugu na jamaa zake.

Jeshi la polisi mkoani humo lililazimika kutuma askari wake baada ya vurugu hizo kudumu kwa saa kadhaa na kuhatarisha usalama wa mganga huyo ambaye anashikiliwa na polisi
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment