-->

HAWA NI MIONGONI MWA WATU WALIONJA CHUNGU YA MWALIM NYERERE KATIKA ZAMA ZA UHAI WAKE

 


1. Idd Amini - Alipoivamia Tz.... Mwalimu alitamka tutampiga nduli!.. Na kweli Idd Amini alipigwa hadi akaikimbia Uganda....

2. Kolimba - Alipotamka CCM imepoteza Dira na Mwelekeo... Mwalimu alimwita Dodoma akamuuliza nani kakutuma useme hivyo?!.. Ndio ukawa mwisho wa Kolimba!..

3. Samweli Sitta - Alipokuwa kiongozi wa serikali ya wanafunzi UDSM aliongoza mgomo wa wanafunzi wenzake kudai siagi na maziwa!... Mwalimu aliibuka pale chuoni akamuuliza Samweli Samweli kwenu mnakunywa maziwa kweli?!.. Akamwambia lala chini, akamcharaza bakora na mgomo ukaishia hapo hapo!...

4. Abdul Jumbe! - Alipotaka serikali tatu!.. Nyerere alimuuliza moja kujumlisha moja ni ngapi?!.. Jumbe akajibu ni mbili!.. Nyerere akamwambia kama ni mbili mbona unataka serikali tatu?!.. Huo ndio ukawa mwisho wa Abdul Jumbe kuwa Rais wa Zanzibar!..

5. John Samwel Malecela - Ni baada ya taarifa kuzagaa kuwa amebadili dini na jina ili apate kuungwa mkono na nchi za kiislamu kugombea Urais mwaka 1995!.. Nyerere alimwambia wee John wewe umeenda Arabuni mara moja umebadilisha jina sasa unaitwa Jumanne!. Ukienda mara ya pili si utabadilisha kabila?!... Huo ukawa mwisho wa ndoto zake kuwa Rais wa Tz !...

6. Edward Lowassa - Alipokodi ndege binafsi ikampeleka hadi dodoma kwenye vikao vya mchujo wa wagombea Urais kupitia CCM mwaka 1995 alimpa lift JK!.. Nyerere alimuuliza mmekuja na Ndege dodoma pesa mmetoa wapi?!.. Jina la Lowassa likakatwa kabla ya vikao vya mchujo!... 

SOURCE:HABARI MPASUKO
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment