SIMULIZI YA ZAMUNDA
Zamunda ni kijana aliyezaliwa Mkoani
Ruvuma wilaya ya Namtumbo katika kijiji cha Liganga. Elimu yake
ya msingi alisoma shule ya Mwembeni na
masomo ya sekondari aliyapata
katika shule ya Kipingo
iliyoko huko mkoani
Ruvuma. Baada ya kuhitimu elimu yake ya sekondari hakupata bahati ya kuendelea na na kidato cha 5 na 6.Kwani daraja lake la ufaulu wake halikuwa zuri la kumwezesha walau kusoma
kozi nyingine ilishindikana. Baada ya
hapo Zamunda alijitosa kwenye
maswala ya kilimo cha Mpunga pamoja na jitihada zake zote lakini jitihada
ilishindwa kuzaa kudra, kwani alichokisudia sio kilicho tokea, Zamunda alipanda
Mpunga ukastawi vizuri sana lakini waswahili wasema lakuvunda
halina ubani,mara tu Mpunga ulipofikia kimo cha kuku jogoo ulianza
kushambuliwa na viumbe waharibifu,mara tu ilipofika mchana kulikuwa na nyani na ngedere wakiuchanachana na kuufyonza kama miwa kwani
mpunga unapofikia kimo hicho cha jogoo huwa
unakuwa na asili ya kuwa na utamu mithili ya sukari guru ndio maana wanyama hao walipendelea kula. Lakini haikukomea hapo tu,kwani kwa wakati wa usiku kulikuwa na wanyama wengine
wahalibifu waliokuwa wakishambulia mpunga kama vile njapuri,mbawala pamoja na
viboko ambao walikuwa wakitokea mto jirani wa Furuwa.
Saa
zilikwenda siku zilipita miezi nayo ikapita takribani
kama miwili hivi, mpunga ukaanza kuchanua punde si punde ukaanza kuiva.kipindi hicho
kilikuwa kikiitwa kipindi cha neema
ngoma nyingi za kimira zilikuwa zikichezwa kama vile Rizombe,unyago,pia
kilikuwa ni kipindi cha watu kuoana
lakini kwa Zamunda kipindi hicho kwake kilikuwa kama shubili kwani ndio
wakati alikuwa akipambana na adha
nyingine ya wan yama na ndege
waharibifu safari hii walikuwa
ndege aina ya njegheya wakishambulia nyakati za mchana
na usiku walikuwa nguruwe,kwa
kweli Zamunda hofu woga kilitawala moyoni mwake kwani
alijiona kama mtu mwenye mkosi ,uchuro ndani ya jamii.Kwa mchakato huo Zamunda hakuweza kupata mavuno
bora ya mpunga kwani hekari
hiyo moja aliweza kupata gunia nne tu badala ya
gunia 20,kwahiyo hapo moja kwa moja alicheza patapotea. Kwani
malengo yake hayakuweza kutimia kutokana
na anguko hilo la kukosa mavuno
ya kutosha.
Zamunda anakuwa mpole mithili ya Bundi wakati wa
usiku amejawa na biwi la mawazo kichwani
mwake juu ya hatima ya maisha yake kwani
kukosa mavuno ni sawa na kukosa
,mahitaji muhimu. Miaka 2 baadae
Zamunda aamua kuachana na kilimo na
kujikita kwenye maswala ya uvuvi katika mto ulio karibu na shamba lake unaoitwa Furuwa. Walahaula walakwata,ni kweli
waswahili husema ng`ombe wa masikini hazai
hata kama akizaa ni tasa; Katika
harakati hizo za uvuvi Zamunda
apata changamoto nyingi. Siku
moja akiwa kwenye shughuli zake za uvuvi
alifukuzwa na kiboko mpaka mtumbwi
aliokuwa akivulia ukapinduka
na kupelekea kuzama .Lakini yeye alikuwa mahili wa kuogelea
aliweza kujiokoa.
Mwaka mmoja baadae Zamunda
aachana na uvuvi na kuamua kutimkia kwa baba yake mdogo wilayani Namtumbo, kijiji cha Ihalinguo huko
anapokelewa kwa shangwe,
bashasha na na
vigegere na babaye pamoja
na familia kwa ujumla.
Lengo la Zamunda kwenda wilayani Namtumbo ni kwa ajiri ya kutafutiwa kazi kwenye kampuni ya
kusindika Tumbaku.Chakushangaza hakuw eza kupata kazi, kwani aliweza
kusota takribani miaka 2 na ushee akiwa
nyumbani mpaka ikafikia kipindi watu
wakimwita majina ya aina mbalimbali ya
kebehi kama vile kulikuwa na baadhi watu wakimwita KKB (kula kulala bule,poyoyo, Bushoke na wengine wakimwita
mototo wa mama. Mchana
unaisha usiku unaingia Zamunda
kwake ni kama mchana usingizi wa
mang`amu ng`amu uliochanganika na mauzauza mengi .sauti
za ndege zikisikika kuashiria kwamba ni asubuhi
ya alfajiri Zamunda anapata lepe la usingizi, sauti ikisikika
kwa mbali kumbe ni ya babaye mdogo
akimtaka aamke waelekee
kazini kwa babaye mara njiani wana kutana na mzee
anayejuana na ba baye.Mzee huyu ni mwanao? Ndio unasemeje? Ninaona kama umejizaa mwenyewe, ndio damu ni nzito kuliko maji .Nusu saa
inapita wanafika kazini kwa babaye mara wakutana
na bosi anatoka akielekea
kwenye mkutano anasimamisha gari akifungua kioo kwa madaha,akimuuliza mzee ni nani huyo
?mzee ajibu ni mwanangu bosi, anakazi?
Baba Zamunda hapana kama utakuwa na kijibarua umesikia
sehemu ninaomba unijulishe maana
anakaa tu nyumbani . Bosi anafikiria kidogo anakumbuka kwamba kuna
rafiki yake mfanya biashara wa mafuta ,anachukua simu yake kwenye boneti ya gari anampigia simu inaita mwishowe inapokelewa halo! Halo! Mbona kimya tupo ila kazi tu za hapa na pale. Bosi sasa kuna kitu ninataka nikuulize , hivi hapo ofisini kwako kunaweza kupatikana nafasi
ya kazi? Ndio ipo nafasi moja tena unabahati sana
nilikuwa ninataka kesho nimwambie
meneja mwajiri atoe tangazo la kuhitaji mfanyakazi.
Baada ya wiki moja Zamunda
anapata kazi ya uafisa
manunuzi kwenye kampuni ya kuuza mafuta ya Superfeo yeye
anakuwa ndio kila kitu kwani kama siku ikatokea hakuwepo
basi manunumzi hayawezi kufanyika.Ni kama usemi unao sema kulala masikini kuamka tajiri, hatimaye
Zamunda anakuwa mtu mwenye
uwezo mkubwa wa fedha
mithili ya bwana Bill geti,
ikapelekea mpaka kujenga majumba ya kifahari
huko kijijini kwao,halafu
akaamua kununua Boti kubwa
ya uvuvi na kuamua
kuanzisha kampuni ya ke ya uvuvi,
ambayo aligharamia vabali /leseni ya biashara hiyo. Kweli Zamumnda aliweza kupata fedha nyingi sana kutokana na Kampuni
yake hiyo ya uvuvi ,kwani
aliweza kupeleka bidhaa zake za
samaki mpaka nchi za nje ,hilo likampelekea kuwa tajiri mkubwa
zaidi mkoani Ruvuma na Wilaya zake
kila ulipofika sehemu yeyote
ile alikuwa akijulikana kama munyu.
Baada ya miaka 5 Zamunda
anatimuliwa kazi kutokana na
kuhujumu kampuni ya Superfeo na kuihimarisha kampuni yake ya uvuvi .Baada hapo upepo mbaya unavuma
kwa bwana Zamunda, kwani
kuanzia hapo hali ya
kifedha na umaarufu ulianza kupungua kwani
maboti yake mengi yalikamatwa
kutoka na na kushindwa kulipia kodi
serikalini, na hatimaye serikali ikaamua
kutaifisha mali yake yote na
yeye kuishia jela ya kifungo cha miaka 2. Ni kipindi
ambacho kigumu sana kwa bwana Zamunda ni majuto, mateso, huko gerezani , lakini kutokana
na msamaha wa Raisi aliweza
kukaa takribani miezi
6 tu na akatolewa na
akianza maisha mapya. Hali
ilkuwa ni mbaya sana kwa
bwana Zamunda hususani
kimaisha, kiafya, ndio
Wahenga husema ‘’mwinyi mwenye
kitu asiye na kitu kidudu cha mwitu’.’
Wiki inapita hatimye Zamunda anazoea
maisha na anafanikiwa kupata kazi ya ulinzi kwenye
kampuni moja ya ulinzi inayoitwa Ukaya
Security company
kutokana kufanya
kazi kwa bidii anateuliwa
kuwa mkuu wa
wa ulinzi wa kampuni hiyo hapo ndipo nyota yake ilipoanza kung`ara tena. Mungu hamtupi mja wake punde si punde saa 2 asubuhi Zamunda anaikuta barua
ofisini kwake aigeuza nyuma na mbele ashindwa kufahamu
kwamba barua imetokea wapi.Aamua kumwita katibu
muhutasi, eti hii barua imetokea
wapi? Sijui kama imetokea wapi
lakini mimi nimepewa na mtu wa
masijala asubuhi na mapema
leo hii. Zamunda anapatwa na mgongano wa mawazo kichwani mwake hivi inawezekana hii barua ni
ya kuachishwa kazi nini?
Mungu wangu nitakuwa mgeni wa
nani mimi.Siku yakwanza inaisha,
siku ya pili jioni karibu na muda wa
kuondoka anapiga
konde moyo anafungua barua inasomeka
kama ifuatavyo “Bwana Zamunda
Shaban kuanzia leo tarehe 12
mwezi wa 1 mwaka 2011 umeteuliwa rasmi kuwa mkuu
wa wa ukaguzi
wa kitengo cha kuzuia
na kupambana na madawa ya
kulevya kilichopo uwanja wa
ndege mjini Songea uteuzi huu unaanza mara moja tunakutakia utendaji mwema katika kazi yako’’. Zamunda akitoka ofisini kwa mbwembwe, madaha ,na furaha iliyojaa
na bashasha , katibu Muhutasi
amuuliza kulikoni Bosi kuna nini
tena? Bosi nimeteuliwa kuwa mkuu wa
ukagazi wa kitengo cha kuzuia na
kupambana na madawa ya kulevya mjini
Songea .Hongera Bosi, hapa tu kwa sasa mambo yako si mabaya sasa ukienda na huko si utanunua
hata gari Moshi?Zamunda hapana itakuwa kawaida
tu kwahiyo unaondoka lini kuelekea huko Songea
mjini? Zamunda ninahisi kesho asubuhi na
mapema nitaondoka.
Zamunda anaripoti kazini kwa mara ya kwanza anapokelewa na kuanza kutambulishwa kwa wafanyakazi wengine .Baada ya mwezi mmoja
maisha ya bwana Zamunda yapo kwenye sayari nyingine ,kwani kila kitu alichokuwa akikitaka alikuwa na uwezo wa
kukipata kwa wakati muafaka Zamunda
aliendelea na kazi yake vizuri
kwenye kampuni hiyo lakini akiwa
kama mkuu wa wa
kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya katika uwanja wa ndege wa mjini songea .Siku moja
askari wasaidizi walifanikiwa kukamata mtu
mwenye mzigo wa madawa ya kulevya kama
kilo hamsini na nusu
wakamfikisha kwa bwana Zamunda
kama mkuu wa wa kitengo Zamunda naye bila ajizi akatoa
taarifa kwa mkuu wa
kitengo cha kuzuia na kupambana
na madawa ya kulevya Tanzania. Yule mtuhumiwa akapelekwa makao makuu mjini Dar es
salaam, kumbe alikuwa ni mtoto mmojawapo wa kigogo wa serikali hapa
nchini Tanzania,
akashitakiwa na hatimaye akakutwa na
hatia mwisho akahukumiwa
kunyongwa kwa kuwa sheria za nchi zilikuwa wazi kabisa, mtu yeyote atakaye
kutwa na hatia ya
kukamatwa na madawa ya
kulevya hukumu yake mtu huyo ni
kunyongwa hadharani , ili iwe fundisho
kwa wengine kwamba kufanya biashara ya
madawa ya kulevya ni hatari.
Zamunda
anaomba likizo kwa ajiri ya kupumzika
anafanikiwa kupata likizo, na akiianza likizo hiyo akiwa nyumbani kwake Mbambabei
sehemu ya watu wazito, ukimya na
upweke katika nyumba ya bwana Zamunda
umetawala, kwani hakuna
sauti za watu bali
ni sauti za panya,
sauti za ndege aina ya Shewele
na madondola ambazo
zilikuwa zikisikika kwa .ukweli
ni kwamba hari ya unyoge na
upweke ulikithiri likizo ya mwezi
ilikuwa kama mwaka mmoja kwa Zamunda , siku kama wiki. Giza
linaingia kila viumbe hai vyarejea makwao,Zamunda naye
anaingia ndani kuikaribisha
siku mpya ,mara anajilaza ubavu,
kifudifudi,chale lakini
usingizi haupatikani
kichwa kimetingwa na mawazo mazito
namna gani anaweza kumpata
mwenza wake? Wiki ya pili imekatika baada ya likizo Zamunda anaamua kupanga
safari ya kwenda Wilayani
Namtumbo kwa baba yake mdogo
kumweleza swala la kutaka mwenza wa kuishinae.Bahati mbaya wazazi
wake wote wawili waliomzaa wameshafariki dunia
kwa ajari ya moto iliyotokea mwaka 1999. kwahiyo mtu aliye bakia wa kumshauri ni huyo tu baba yake mdogo mzee Kimbyoko.
Siku ya jumatatu asubuhi
na mapema Zamunda anajihimu kwenda kukata tiketi ya basi kwa ajiri ya
safari ya Namtumbo.
Anafanikiwa kupata tiketi ya basi
la Super feo.Asubuhi na
mapema Dereva anampitia tayari kwa
kumpeleka kituo cha mbasi,
Zamunda akiendelea kupanga nguo zake kwenye mabegi,Dereva apiga honi
pipiiiiiiiiiip pipiiiiiiiiiiip
pipiiiiiiiii Zamunda amkalipia mlinzi
mbona haufungui geti wewe bwege? Mlinzi samahani
bosi nilikuwa nimepitiwa na usingizi kidogo, mlinzi anafungua
geti Dereva anakwenda mojakwamoja
Sebuleni anakutana uso kwa
uso na
Zamunda ,Ohoooo!!1! umefika
Dereva? Ndiyo Bosi,shikamoo!!Zamunda
marahaba. Dereva vipi upo tayari bosi?
Bosi ninamalizia kupanga nguo kidogo,mara Dereva anamwomba bwana
Zamunda amsaidie maana anahofia wasije kuchelewa basi kituoni, ndani ya mabegi kumepakiwa zawadi kedekede,kuna makoti ya baridi ya baba
yake,kanga,kaniki, kiko ,pamoja na kisu cha babaye cha kuchongea mianzi kwa
ajiri ya kutengenezea vikapu na vitunga. Dereva anamfikisha stendi anakuta basi halina mtu hata mmoja ndani yeye ndio anakuwa wakwanza
,kondakta anamsaidia kuweka mizigo mikubwa ndani buti la basi anabaki na kidadavuzi mpakato(laptop) muda wa kuanza
safari umewadia ni saa 1:30 asubuhi Dereva anaingia ndani ya gari anawasha gari
na kupiga honi nyigi za fujo
akimaanisha kwamba muda wa kuondoka umefika abiria waingie ndani ya basi abiria wanaingia ndani ya gari
kondakta anaamuru abiria wote wafunge
mikanda ,mara safari inaanza mnamo wa saa
1:40 hivi .
Zamunda anapata bahati ya kukaa na
na msichana mrembo,msichana ambaye
ni mweupe pee,mwenye macho ya
kurembua , ngozi tefutefu,nywele ndefu mithili ya singa, sifa
hizo zote Zamunda alishindwa
kubandua jicho lake kwa mrembo huyo.safari
inaendelea mbuga na mbuga,vijiji kwa
vijiji wanavipita.Muda wote huo
wakiendelea na safari hakuna hata mmoja kati yao aliye msalimia mwenzake.Zamunda
aamua kuweka visikilizio(head phone)
zake masikioni huku akicheki movi kwenye
kidadavuzi chake mpakato sauti akiiondoa
kwa ajiri ya kuepusha kero kwa abiria wenzake, mara binti alipitiwa na usingizi,hamadi kibindoni anastuka
usingizini anamwona Zamunda anaangalia muvi kwenye kidadavuzi mpakato, hatimaye binti
baada ya kunata, maringo na
mbwembwe nyingi mara anaamua kumwita
Zamunda hiyo ilikuwa baada ya
kufika kituo cha mabasi .Binti samahani
kaka unaweza kuniangalizia vocha
hapo nje labda kuna wauza
vocha? Zamunda anafungua dirisha na anaangaza
macho huku na kule bila mafanikio,amgeukia dada na
kumjibu hakuna muuza vocha dada, bali
kuna wauza mahindi ya kuchoma tu ndio ninaowaona hapa, Dada oh!! ni kweli
siku ya kufa nyani miti yote huteleza ,sijui nitafanyaje vocha
nimeishiwa ninakoenda pia sijawahi kufika siku hizi za
karibuni tangu nitoke mdogo. Baada ya
muda Zamunda anarudisha visikilizio (head phone) zake masikioni
akiendelea kula ngoma na
kuangalia muvi kwenye kidadavuzi
chake mpakato . Baada ya masaa mawili
Zamunda anafungua dirisha mara anaona bango la kampuni
ya simu za mikononi Airtel
likionesha umbali kwa kilomita bango hilo lilionesha kilo mita 150 zimebaki kufika kijijni kwao Lihuli. Punde akamuuma sikio binti
tunakaribia kufika safari yetu,
Binti umejuaje ndugu? Zamunda
nimetazama kibao kinachoonesha
umbali kwa kilomita. Binti akiwa na wasiwasi akamgeukia Zamunda na kumwomba
msaada wa simu ya Zamunda ili
ampigie mweyeji wake kumjulisha
kwamba anakaribia kufika
ili amsubili kituo cha mabasi.
Ile anamalizia tu kuzungumza na mwenyeji
wake mshindo mkubwa unatokea mithili
ya bomu,gari ikaanza kuyumba huku
watu wakipiga mayowe kama vile
mama!!!!!!!!!!tuna kufa!!!! Dereva
simamisha gari tunakufa
kwa
bahati nzuri dereva anafanikiwa
kusimamisha gari yeye, kondakta na abiria wote wana
teremka chini haraka wanagunda mlio ulikwa wa mpasuko wa taili.Muda wote wa myumbo huo wa gari binti alikuwa amemkumbatia Zamunda
kifuani kutokana na woga .Mungu
mkubwa hapakuwa na mtu yeyote
aliyeumia wala kufa .
Zamunda
anamgeukia binti na kumuuliza umeumia ndugu? Binti wewe je?
Zamunda mimi mzima ninamshukuru mungu sijaumia, binti
kwa sauti ya chini akisikika akimwomba
msamaha Zamunda , ila samahani kaka ninaomba nikufute hapo kifuani labda nimechafua shati yako nyeupe, binti anatoa kitambaa kutaka kufuta sehemu iliyochafuka kwa jasho. Zamunda amzuia
Binti, we acha tu dada usijari kwani
hukujiandaa kunichafua ila imetokea tu
bahati mbaya . Binti atoa asante
ya kimahaba huku sauti ikitokea puani
huku dereva na kondakta
wakihangaika kubadilisha mataili ya gari.Chini
ya kivuli cha mti wameketi
wakisubiri kubadirishwa kwa mataili
Zamunda na binti wanaanza kujitambulisha kila mmoja.Zamunda
wewe unaitwa nani? Binti akitoa biskuti pamoja na soda aina ya Azam embe akimpa Zamunda, lakini Zamunda anaonesha kusita kupokea na kumwambia
binti kwamba sipokei mpaka uniambie unaitwa nani,Binti kwa sauti ya mahaba
usijari nitakuambia mpendwa
pokea kwanza .Zamunda apokea. Dakika mbili baadae
binti anamwambia Zamunda mimi ninaitwa Kachiku ni
mzaliwa wa huku Namtumbo. Zamunda hata mimi pia ni mzaliwa wa
huku. Zamunda hakuisha hamu akauliza
swali jingine kwa binti
huyo mrembo alimuuliza tena, je umeolewa Kachiku au unamchumba? Kachiku
sijabahatika kwa hayo yote mawili.
Takribani lisaa limoja na nusu limepita kondakta
anawatangazia abiria kuingia ndani
ya gari tayari
kwa kuendelea na safari yao ya
kuelekea Namtumbo vijijini.safari inaendelea dereva anapangua na kutia gia moja baada ya nyingine.Hatimaye Kachiku
anakumbushia ombi lake la
simu kumpigia mwenyeji wake,
Zamunda bila kufanya ajizi anampunguzia salio la shilingi 5000. Kachiku
haamini kilichotokea anamshukuru
sana Zamunda hatimaye Kachiku
anawasiliana na mwenyeji wake .Nusu saa
baadae Kondakta anatangaza vituo vya kuteremka abiria,mara tu Zamunda
akamuuliza kachiku unateremkia wapi? Nitateremkia mwisho wa gari. Zamunda sote basi tutateremkia sehemu moja ,kondakta arudia kutangaza abiria tumeshafika kituoni hapa ndio mwisho wa gari.Zamunda na Kachiku wanateremka
wanaagana kila mmoja anaelekea
upande wake. Punde si punde Kachiku
analakiwa na mwenyeji wake ,Zamunda anachukua Bodaboda kumpeleka nyumbani kwao.Zamunda afika kwao
kwa babaye mdogo akilakiwa
kwa bashasha kubwa
mno, huku wakimpokea mizigo
na kupeleka ndani ambako atalala.Mama mdogo akifanya maandalizi ya
chakula cha mgeni baba
akiongea na Zamunda . Ghafla anapita jirani kuelekea kugema ulanzi,baba Zamunda anamwita jirani, njoo
jirani umuone mwanangu
lakini siyo bure unatakiwa
ulete mbeta(chupa) mbili za ulanzi? Jirani anafika anasalimiana na
Zamunda,baada muda jirani
anatoweka.
Baada ya ukimya wa muda
kidogo Zamunda anafikwa
na mawazo kichwani mwake wazo hilo si linguine ni swala la mke, na
kuanza kumweleza baba yake mdogo “baba safari yangu ya kuja huku
siyo kukuoneni ninyi tu
la hasha nina jambo
ninataka nikuambie ‘’. Baba anahamaki huku masharubu
yake yakicheza cheza mithili ya
paka dume, nini tena mwanangu umepata balaa gani tena?Umerogwa nini? Hapana baba ninataka niwe na mwenza ,baba mwenza ndio
nini? Ninataka kuoa.Baba anafikiria
kwa muda na kisha anavuta pumzi
kwa kasi mithili ya baiskeli iliyopata pacha ghafla. Baba Zamunda mimi nilikuwa na mawazo kama ya kwako kila siku
nilikuwa ninajiuliza lakini
nilikuwa sipati jibu maadam
mwenyewe umetamka basi hakuna
shida,kwakuwa leo umechoka na
safari nenda kapumzike tutaongea
kesho.Siku mpya imeanza asubuhi na
mapema baba ana mgongea Zamunda za
asubuhi mwanangu umeamkaje? Zamunda nimeamka
salama baba. Mara anatoka nje
anasalimiana na baba yake mdogo na mama yake mdogo pia. Wakiendelea na
mazungumzo asubuhi hiyo mara ghafla anapita Kachiku
pamoja na mtoto wakienda kisimani kuchota maji,Kachiku anasalimia wazazi wa Zamunda,ghafla anagongana macho na Zamunda, Kachiku anaacha ndoo
ya maji chini na kwenda kumsalimia kwa karibu, Kachiku anashikwa na mshangao
baada ya kumuona Zamunda kumbe
unakaa hapa mpendwa? Kumbe ni majirani mimi ninakaa pale nyumba ya tatu kutoka
hapa, karibu nyumbani basi kaka
. Zamunda usijali nitakutaarifu kama lini nitakuja kwa kuwa namba yako ya simu ninayo hakuna shida.Usiku umeingia Zamunda anampigia simu Kachiku
simu inaita kwa muda mrefu hatimaye inapokelewa haloo! Nani mwenzangu?Mie Zamunda unakumbuka asubuhi ulipita nyumbani kipindi unakwenda kuchota
maji , Kachiku enhee! Nimekumbuka mambo vipi? Zamunda
poa, lakini nina jambo ninataka
kukuambia unaniruhusu? Kachiku uwe huru,unakumbuka kipindi
tulipokuwa tunasafiri kuja
huku Namtumbo nilikuuliza
umeolewa? Nawe ukanijibu hapana !
Sasa mimi ninaomba uwe mke wangu wa
ndoa je wasemaje? Kachiku apatwa
na mshituko na kigugumizi kwa ghafla,
na akiuliza unayosema ni ya kweli
au* photocopy*?Zamunda ni kweli
zahiri shahiri.Hatimaye Kachiku akubali
maombi ya bwana Zamunda .
Usingizi mmoja umeisha asubuhi imewadia Zamunda
anakuwa wa kwanza kuamka tofauti
na siku za nyuma
mpaka baba yake akashangazwa na
hali hiyo, leo kulikoni mbona umeamka
mapema sana? Baba nina habari njema. Habari gani hiyo?Yule binti aliyetusalimia jana
ndio mkamwana wako ninataka kumuoa .Baba hakuna shida we maadam kama umeelewana nae sisi ni watu wa
kukusikiliza wewe. Mipango ya kwenda kujitambulisha kwa wazazi
wa Kachiku inafanywa
hatimaye baada ya muda ndoa
inafungwa .Zamunda anapata mke, mara
likizo inaisha anaondoka na mkewe akirudi
Songea mjini kuendelea na kazi. Zamunda anafika songea mjini
siku ilyofuata asubuhi na
mapema anajiandaa kwa ajiri ya kwenda
kazini, mara dereva anapiga honi mlinzi
anafungua geti. Dereva anaingia sebuleni
kwa kumsubiria bwana Zamunda,mara
Zamunda anatoka karibu Dereva, habari za siku, wanashikana
mikono .Zamunda safari hii nimekuja na
shemeji yako, Dereva ahaa!!! Yuko wapi ? yupo ndani anavaa tumetoka kuoga atakuja punde tu.
Kachiku anatokea na kuanza kusalimiana
na Dereva.Zamunda anaondoka na
Dereva kuelekea kazini, na kuanza maisha mapya ya mke na
mume.
MWISHO
0 comments :
Post a Comment