-->

ZITTO KABWE AFUNGUKA CHANZO CHA TOZO YA SIM CARD

Hii ni nukuu ya post ya Mheshiwa Zitto Kabwe katika facebook
 
#‎simcardtax‬ NINI KILITOKEA?

Finance Act, section 11 6(C) introduces #simcardtax

"(6C) There shall be charged an excise duty on telecommunication sim card at the rate of shillings 1,000/= per month."

Kifungu cha 11 kinaongeza kifungu cha 6C kwenye kifungu cha 124 cha Excise (Management and Tariff) Act CAP 147. Kwa kiswahili

"kutakuwepo na tozo la ushuru wa bidhaa (excise duty) la Tsh 1,000 kwa mwezi kwa kwa kila SimKadi"

Nini kilitokea? (What transpired)

Mwishoni mwa mwaka jana, 2012, Spika Anna Makinda aliunda Kamati ya kufanya uchunguzi kuhusu vyanzo vya mapato ya Serikali. Kamati ili iliongozwa na Mbunge wa Bariadi ndugu Andrew John Chenge. Moja ya mapendekezo ya kamati ile ni kuanzishwa kwa kodi hii ya simkadi. Taarifa ya kamati ile ilipelekwa Serikalini na haikuwahi kujadiliwa na Bunge (licha ya rasilimali fedha ya Bunge kutumika kuendesha kamati ile).

Waziri wa Fedha, ndugu Mgimwa, alipokuwa anasoma Hotuba ya Bajeti mwezi Juni mwaka 2013, alitamka kuwa kifungu cha kuanzishwa kodi hiyo hakipo tena (ilikuwa tshs 1470 kwa mwezi). Kifungu hiki kilikuwa kwenye hotuba yake. Inaonyesha kuwa huko Serikalini hawakuelewana kuhusu jambo hili na hivyo kuamuriwa kufutwa (kulikuwa na Baraza la Mawaziri asubuhi ya siku Bajeti inasomwa).
Hivyo pendekezo hili halikujadiliwa kabisa na Bunge kwenye mjadala wa Bajeti ya Serikali na KWA HIYO halikupitishwa kwenye Makadirio ya Mapato ya Serikali.

Baada ya Bajeti kupita, Bungeni huletwa miswada 2, mmoja ni mswada wa matumizi (appropriation bill) na mwingine ni muswada wa mapato (Finance bill). Katika muswada wa Mapato hapakuwa na kifungu cha kutoza kodi hii ya simkadi.
Wizara ilipoenda kwenye Kamati ya Bajeti, ili kupitia muswada huu, Kamati ya Bajeti ikahoji ni kwa nini pendekezo lake limekataliwa na Serikali? Hatimaye Kamati ya Bajeti ikashinda na kifungu cha kodi ya simkadi kikaingizwa kwenye muswada wa Fedha 2013/14 kupitia jedwali na marekebisho.
Baadhi ya wabunge kama John Mnyika waliandika jedwali la marekebisho kupinga pendekezo hili lakini kwa kuwa majedwali yote yalikuwa yakiishia kwenye kamati ya Bajeti ya Bunge, marekebisho yao yakagonga mwamba.
Hatimaye Bunge lilipitisha Muswada huu na kuwa Sheria.

Nadhani kwa umuhimu wa historia ni vema kupata hansards za mjadala mzima wa sheria ya Fedha mwaka 2013/14 ili kuweka kumbukumbu ya mbunge gani alichangia nini na namna gani sheria ilipitishwa kifungu kwa kifungu. Pia ni muhimu sana kujiuliza ni kwa nini baada ya sheria hii kupita tarehe 29 Juni mwaka 2013, kulikuwa na ukimya mkubwa na hakuna aliyepaza sauti mpaka wananchi walipoanza kuhoji kupitia mitandao ya kijamii.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment