1. Kama taarifa zote zilizoko kwenye mtandao wa wikipedia zingeandikwa kwenye kitabu, hiko kitabu kingekuwa na kurasa milioni mbili nukta tano na ingemchukua mtu wa kawaida hadi miaka 123 kumaliza kukisoma mwanzo hadi mwisho.
2.Magereza nchini Brazil yana utaratibu wa kuwapunguzia wafungwa wake vifungo vyao kwa siku nne kwa kila kitabu maalum ambacho mfungwa anamaliza kukisoma, yaani ukimaliza kusoma kitabu kimoja kizima kifungo chako kinapunguzwa kwa siku nne.
3.Jose Alberto Mujica ambaye ni rais wa Uruguay anashikilia rekodi ya kuwa rais mwenye kipato cha chini kuliko wote,rais huyu hujitolea asilimia 90 ya mshahara wake kusaidia watu wasio na uwezo.
4.Kuna mtu aliyefahamika kama Michael Tolotos ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 80, cha ajabu kumhusu mtu huyu ni kwamba mpaka anafariki dunia hakuwahi kumuona mwanamke, imetokea tu na wala hajawahi kuwa kipofu.
5. Panya wa kike wana uwezo wa kuzaa watoto mpaka 100 kwa mwaka mmoja.
0 comments :
Post a Comment