Neymar ashinda tuzo ya mchezaji bora
Mshambuliaji huyo wa Brazil alifunga katika mechi nne kati ya tano zilizochezwa na timu hiyo kwenye dimba hilo na kujipasha moto kwa ajili ya Kombe la Dunia, ikiwa ni pamoja na goli moja katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Uhispania Jumapili katika fainali.
Kiungo wa kati wa Uhispania Andres Iniesta alipokea Silver Ball (Tuzo ya Nambari ya Pili), naye kiungo wa kati wa Brazil Paulinho akapokea Bronze Ball (Tuzo ya Nambari ya Tatu).
Mshambuliaji wa Uhispania Fernando Torres alishinda tuzo ya mfungaji bora wa mabao, Golden Boot, baada ya kufunga mabao matano kwenye dimba hilo. Fowadi wa Brazil Fred alikuwa wa pili na Silver Boot, akiwa pia na mabao matano lakini akiwa amecheza muda zaidi. Neymar alifunga mabao manne na akajishindia Bronze Boot.
Pia, golikipa wa Brazil Julio Cesar alishinda tuzo ya mlinda lango bora wa dimba, Golden Glove, nayo Uhispania ikatwaa tuzo ya Fair Play kwa mchezo wake bora.
0 comments :
Post a Comment