Rais
Jakaya Kikwete na rais wa serikali ya mpito ya Madagascar,Mh Andry
Rajoelina wamekutana kwa mazungumzo ya muda mrefu kuhusu mgogoro wa
kisiasa katika Kisiwa hicho kilichopo bahari ya Hindi na njia za kuweza
kutatua mgogoro huo wakati nchi hiyo ikijiandaa na uchaguzi mkuu.
Kwa
mujibu wa taarifa ya kurugenzi ya mawasiliano ya rais Ikulu mazungumzo
hayo rais Rajoelina na rais Kikwete yaliyochukua zaidi ya saa moja
yamefanyika Ikulu jiji Dar es salaam na zaidi yalilenga kumuomba rais
Kikwete ushauri kukabiliana na hali ya kisiasa nchini mwake..
Rais
kikwete katika mazungumzo hayo ametumia muda kumweleza rais Rajoelina
jinsi Tanzania, nchi nyingine ikiwamo Jumuia ya maendeleo Kusini mwa
Afrika (Sadc), Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya ya Ulaya(EU) zinavyoina
hali ya Madagascar na njia zipi zinaweza kutumika kutatua mgogoro wa
kisiasa.
Rais kikwete ambaye ni mwenyekiti wa
asasi ya siasa, ulinzi na usalama (Troika-organ) ya Sadc ndiye amepewa
jukumu na viongozi wenzake wa sadc kutafuta majawabu katika migogoro ya
kisiasa inayozikabili nchi wanachama wa Sadc ikiwamo Madagascar, Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na ZimbabCREDIT TO:ITV
0 comments :
Post a Comment