Kwa ufupi
- Licha ya mimi kutokuwa na cheo pale, lakini hili la kutukagua na mbwa, ni kama wametudhalilisha... sisi ndiyo tunaaminika kwa usalama, leo hii wanatukagua na mbwa. Tena Kituo Kikuu.”
Tukio hilo lilitokea muda mfupi kabla ya msafara
wa magari ya Marekani kupita yakitokea Ikulu kwenda Uwanja wa Ndege wa
Julius Nyerere kumlaki Rais Barack Obama.
Polisi ambaye hakutaka kutajwa alisema ofisa huyo aliingia na mbwa hadi maeneo ya mapokezi, lakini muda mfupi walitoka.
“Walikwenda moja kwa moja mapokezi wakafanya
ukaguzi, kisha wakatoka nje ya jengo na kama hiyo haitoshi, ofisa huyo
akiwa na mbwa alikwenda sehemu ya kuegesha magari yenye kesi na yale ya
kawaida na kuanza kufanya ukaguzi, baada ya hapo waliondoka,” alisema
polisi huyo na kuongeza:
“Licha ya mimi kutokuwa na cheo pale, lakini hili
la kutukagua na mbwa, ni kama wametudhalilisha... sisi ndiyo
tunaaminika kwa usalama, leo hii wanatukagua na mbwa. Tena Kituo Kikuu.”
Hata hivyo, usalama kwenye vituo vingi ikiwamo
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juliusu Nyerere, vilikuwa chini ya
usimamizi na uangalizi wa makachero wa Marekani.
habari kwa ihsani mwananchi
habari kwa ihsani mwananchi
0 comments :
Post a Comment