-->

DONDOO ZA AFYA:VYAKULA VINAVYOSHAULIWA KWA WATOTO WENYE UMRI WA MIEZI SITA

Mara nyingi tumekuwa tukishauriwa kuwaanzishia watoto wetu chakula cha ziada tofauti na mziwa ya mama pale wanapofikisha umri wa miezi sita kwa ajili ya ukuaji mzuri. Vyakula unavyoshauriwa kumpa mtoto wako katika kipindi hiki ni vile vyenye uwezo wa kumeng'enywa kirahisi, virutubisho vya kutosha pamoja na kiasi kidogo cha chumvi na sukari kwani huweza kusababisha madhara afya ya kibofu na meno.

Unaweza kumsagia karoti, viazi, wali, ugali,  karanga,papai, nanasi na nyama nyekundu humpatia mtoto nguvu, vitamini, protini, nyuzinyuzi na madini muhimu katika ukuaji asa vinapotumika kwa mpangilio.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment