IMBA ASISITIZA WANA KIKOSI BORA KULIKO YANGA, ATOA SABABU TATU
TULLY (KULIA), AKIZUNGUMZA NA KOCHA MKUU WA ORLANDO PIRATES, VLADIMIR VERMOZOVIC RAIA WA SERBIA. |
Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Simba, Said Tully amesema wao wana kikosi bora kuliko Yanga kutokana na sababu tatu alizozitaja.
Moja:
Tully
amesema wanakutana na kikosi cha Yanga chenye beki mbovu ambayo
imeruhusu bao katika kila mechi ikianza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya
Mtibwa Sugar.
Mbili:
Yanga imepoteza mechi moja, Simba haijapoteza hata moja, ingawa imetoa sare mechi tatu.
Tatu:
Yanga
wana fowadi iliyofunga mabao manne katika mechi tatu, haikufunga katika
mechi moja, hivyo si ya kuilinganisha na ile ya Simba iliyofunga bao
kila mechi.
Tully ametamba kwamba Simba imekuwa ikiinyanyasa Yanga inavyotaka kwa kuwa ina kikosi bora.
"Tunaiheshimu
Yanga kama mtani wa jadi, lakini sisi tunajiamini kuwa kikosi chetu ni
bora zaidi ya Yanga, nazungumzia kwa maana ya ufundi na si ushabiki.
"Hilo linajulikana na liko wazi, mashabiki wa Simba waje uwanjani kesho, kikubwa waiiunge timu mkono," alijigamba Tully.
Mjumbe
huyo wa kamati ya utendaji alikuwa mmoja wa viongozi walioambatana na
timu nchini Afrika Kusini ilikoweka kambi na kucheza mechi tatu za
kirafiki ikipoteza mbili na kutoka sare moja.
0 comments :
Post a Comment