Kiboko yao: Cristiano Ronaldo amefunga mabao mawili dhidi ya Chelsea
KIUNGO
Frank Lampard alicheza kwa mara ya kwanza majira haya ya joto, lakini
alishindwa kumzuia Cristiano Ronaldo kuinyanyasa Chelsea jana.
Kabla
ya mechi hiyo na Real Madrid mjini Miami, kiungo huyo mkongwe alikosa
mechi zote za kujiandaa na msimu za klabu, Stamford Bridge kutokana na
kuwa majeruhi.
Lakini
Lampard ameimarika na kuanza kazi tayari kwa mchezo wa kwanza wa Ligi
Kuu dhidi ya Hull City, Agosti 18 baada ya kumaliza dakika 45 za kwanza
katika Fainali ya Mabingwa wa Kimataifa wa Guinness.
Katika
mechi hiyo, mabao mawili ya Ronaldo na moja Marcelo, yalitosha
kuitotesha timu ya Jose Mourinho 3-1 dhidi ya timu yake ya zamani ambayo
kwa sasa inafundishwa na Carlo Ancelotii.
Mazungumzo
baada ya tukio: Mourinho na kocha wa zamani wa Chelsea, ambaye kwa sasa
ni kocha wa Madrid, Carlo Ancelotti wakizungumza baada ya mechi
Mapenzi yameisha: Shabiki la Real Madrid likiwa limebeba bango kuonyesha kutojali kuondoka kwa Mourinho katika klabu hiyo
Mabingwa: Nyota wa Real Madrid wakisherehekea kuifunga Chelsea katika fainali ya Mabingwa wa Kimataifa wa Guinness
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas, Arbeloa, Pepe, Ramos, Marcelo, Modric, Khedira, Isco, Ozil, Ronaldo na Benzema.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Terry, Cahill, Cole, Lampard, Van Ginkel, Ramires, Oscar, Hazard na Lukaku
0 comments :
Post a Comment