Mwili wa mwanafunzi huyo ukishushwa kutoka chumba alichokuwa amelala. |
Mwanafunzi huyo wa mwaka wa pili aliyekuwa akichukua Shahada ya kwanza ya Biashara na Uhasibu, baada ya kutoka darasani alikwenda kupumzika na hakuamka tena.
Habari za ndani kutoka kwa marafiki zake zililiambia NIPASHE kuwa mwanafunzi huyo alitoka
darasani majira ya saa 5 asubuhi na kuwaomba wenzake wamuamshe saa 6 mchana baada ya kupumzika.
Chanzo chetu cha habari kilisema kuwa wanafunzi wenzake walipokwenda kumwamsha, alikuwa amekwisha fariki dunia.
Shuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazeti, alisema Happiness alihudhuria vipindi vya asubuhi na baada ya kutoka darasani aliwaambia wenzake kuwa anakwenda kupumzika.
Nickson alisema wanafunzi walitoa taarifa kwa madaktari wa chuo na ndipo mwili huo ulipochukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi.
Alisema madaktari wanasubiri ndugu wa marehemu kwa ajili ya kuufanyia uchunguzi mwili huo leo na taarifa ya sababu ya kifo hicho itatolewa. Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Thobias Tedoyeka, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Alisema maafisa wa polisi wapo chuoni hapo kwa ajili ya uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo hicho.
Beatrice Shayo, NIPASHE, Dar es Salaam.
0 comments :
Post a Comment