-->

KISA CHENYE MAFUNZO(VOL 26) KIJIJI NA ASALI

KISA CHENYE MAFUNZO(VOL 26)
Kijiji kimoja katika utawala kilikuwa kikiongozwa na mfumo wa kifalme,Baada ya mfalme wa kwanza kufa ikadi achaguliwe kiongozi mpya yaani mfalme mpya.
Yule mfalme baada ya kupewa uongopzi aliwashukuru sana wananchi kisha akawauliza je kama nikiwaagiza mtakuwa mkitenda ntakachokisema?
wananchi:ndiooooooooooooooooooo
kiongozi:je mtakuwa waaminifu kwangu?
wananchi:ndioooooooooooo
kiongozi:je mtakuwa watiifu kwangu?
wananchi:ndioooooooooooooooooo
kiongozi:Ili nifahamu haya niliyowauliza nitawaagiza jambo kisha hilo litanipa jawabu zaidi kuliko haya maneno yenu.
Yule mfalme mpya akaagiza kila mwanchi mtu mzima abebe kikombe kimoja cha asali kutokea nyumbani na kuja kuweka kwenye pipa la mfalme.Mfalme alilichukua lile pipa na kuliweka sehemu ya wazi bila ya kuchunguza jinsi ya wanavyoweka.
Wananchi wachache walileta vikombe vyao asali kama alivyoagiza mfalme,lkini wengi wao walileta maji baadala ya asali huku kila mmoja akihisi kwamba kwa kuwa watu woote wataleta asali hivyo yeye akileta maji hakuna atakae jua.
Na mwisho wa yote pipa lilijaa maji na asali kidogo iliyowekwa na watu wachache.
FUNZO:Kila mmoja akisema hili litafanywa na fulani mwishoe jambo halitafanyika
SHARE KAMA UMEIPENDA,WEKA COMMENT KAMA UMEGUSWA AU BOFYA LIKE KUONYESHA TUKO PAMOJA
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment