Zikiwa
zimebaki siku 29 kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la dunia mwaka
2014 kuanza, usalama bado umeonekana kuwa tatizo nchini humo.Mapema wiki
hii kwenye mitandao tofauti nchini humo imeonekana video moja
ikionyesha mchezo wa timu za mchangani, ambapo adhabu ya penati
iliyotolewa na mwamuzi ilisababisha vurugu zilizohusisha silaha kali
kama bunduki AK-47.
Watu kadhaa waliokuwa wamevalia jezi za timu ya taifa ya Brazil
wakiwa na silaha zao walianza kurusha risasi juu kwa muda usiopungua
sekunde 35.
Tukio hilo lilitokea kwenye eneo la Bangu, magharibi mwa mji wa Rio de Janeiro. Angalia video……….
0 comments :
Post a Comment