-->

HUYU NDIO RAISI WA NCHI ALIESAJILIWA KUCHEZA MPIRA WA MIGUU

http://img.timeinc.net/time/daily/2007/0705/bolivia_postcard_0531.jpg
Nikikupa nafasi ya kuniambia namba ngapi atakua anacheza huyu president wa nchi kwenye hili soka unaweza kuotea ?.
 
Sasa unaambiwa club moja huko Bolivia (Sports Boys) imemsajili rais wa Bolivia Evo Morales kucheza kama kiungo wa kati kuanzia Agosti 2014 na mgongoni atakua na jezi namba 10 huku mshahara wake kwa mwezi ukiwa ni dola za Kimarekani 213 kwa mwezi ambazo ni zaidi ya laki 3 za Kitanzania.http://api.ning.com/files/ewtvLniYpoPok3BW0vImFtZyuHEELH6a*a0ilascsbA-q2eHCBZvsAPnIKm6Q8nPbhRqDtfevadA6kMErEOov1tEVdLIssjJ/EVO.jpg
Kwa sasa mashabiki wanamsubiri president huyo mwenye umri wa miaka 54 ambae ni shabiki mzuri soka na atakua akiichezea Sports Boys ikiwa ni timu iliyopo kusini mashariki mwa mkoa wa Santa Cruz.

Timu hiyo ambayo ipo katika ligi ndogo imesema rais huyo atakuwa akicheza kwa dakika 20 katika kila mechi watakayokuwa wanacheza hasa ikizingatiwa kuwa ni mtu mwenye shughuli nyingi.
EVO MORALES SOCCER 
Rais Morales amewahi kucheza katika mechi nyingi pamoja na wanahabari, viongozi wa umoja na marais wengine huku kumbukumbu ikionyesha mwaka 2007 rais huyo alishiriki katika mechi iliyokusudiwa kupinga kikwazo kilichokuwa kimewekwa kwa Bolivia cha kutoshiriki katika mechi za kimataifa.

Mwaka 2006 alipata matatizo uwanjani kwa kuvunjika mguu wakati alipogongana na kipa.
CHANZO millardayo.com
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment