taiRi ya bajaji hiyo likiwa limekatika |
Askari wa usalama barabara wakikagua ajali hiyo mbaya iliyosababisha hadi ukuta wa uzio wa bustani ya Manispaa ya Iringa kubomoka |
Bajaji ikiwa imepata ajali mbaya mchana huu eneo la posta mjini Iringa |
Bajaji ya Mng'aro wa sembe akiwa emepata ajali wakati ikisambaza unga huo |
Wananchi wakishuhudia ajali hiyo mbaya |
Maneno ya maudhi yaliyoa ndikwa nyuma ya Bajaji 'FUATA YAKO" nusuru yamtokee puani dereva
BINTI
mmoja ambae ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari mjini Iringa
amejeruhiwa vibaya baada ya kugongwa na Bajaji ya kampuni ya unga ya
Mng'aro wa Sembe ya mjini hapa.
Ajali
hiyo imetokea majira ya saa 8.35 mchana wa leo katika eneo la Posta
barabara ya Iringa- Dodoma wakati Bajaji hiyo ikitokea eneo la
Kihesa kuja mjini Iringa.
Mashuhuda
wa ajali hiyo wameueleza mtandao huu wa matukiodaima.com kuwa
chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambao dereva wa bajaji .
Kwani alisema iwapo dereva huyo angekuwa katika mwendo wa kawaida ajali hiyo isingetokea.
Hata
hivyo mashuhuda hao akiwemo Bw Mashaka Kayoka ambae ni mmoja kati ya
wauza magazeti maaarufu eneo hilo la posta alisema kuwa binti huyo
ni mtu pekee aliyejeruhiwa japo eneo hilo huwa wanashinda watu wenye
ulemavu wa viongo wakijishughulisha kwa biashara ila wamenusurika .
Mbali ya mwanafunzi huyo kujeruhiwa hakuna mtu mwingine aliyejeruhiwa na dereva wa bajaji hiyo amekamatwa .
Kwa hisani ya matukiodaima.com
0 comments :
Post a Comment