Wachezaji
wa kimataifa wa Tanzania wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC), Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu
wanatarajiwa kuwasili Jumamosi mchana (Mei 17 mwaka huu) kujiunga na
Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi ya Zimbabwe (Mighty Warriors).
Washambuliaji
hao watatokea moja kwa moja Sudan ambapo kesho (Mei 16 mwaka huu) TP
Mazembe itacheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya timu ya huko.
Ujio
wa washambuliaji hao utafanya wachezaji wote kutoka nje walioitwa na
Kocha Mart Nooij kuwa wamepatikana kwa ajili ya mechi hiyo ya mchujo ya
Kombe la Afrika ambalo fainali zake zitachezwa mwakani nchini Morocco.
Mchezaji mwingine wan je ambaye tayari ameripoti Stars ni Mwinyi
Kazimoto anayecheza nchini Qatar.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linamshukuru Mmliki wa TP Mazembe
ambaye pia ni Gavana wa Jimbo la Katanga, Moise Katumbi kwa kuwaruhusu
wachezaji hao kujiunga na Taifa Stars kwa vile mechi dhidi ya Zimbabwe
ipo nje ya kalenda ya FIFA.
Naye
Kocha Nooij atakuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho (Mei 16
mwaka huu). Mkutano huo utafanyika saa 5 kamili asubuhi kwenye kambi ya
Taifa Stars iliyopo katika hoteli ya Accomondia.
Wakati
huo huo, Zimbabwe inawasili usiku wa kuamkia Jumamosi (Mei 17 mwaka
huu) ikiwa na msafara wa watu 27. Timu hiyo itatua saa 7.30 usiku kwa
ndege ya Ethiopian Airlines na itafikia hoteli ya Sapphire Court iliyopo
Mtaa wa Lindi, Dar es Salaam.
Zimbabwe
itafanya mazoezi siku hiyo jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa Jumapili saa 10 kamili jioni kwenye
uwanja huo huo.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments :
Post a Comment