KISA CHENYE MAFUNZO(VOL 17)SI ANAEWAZA ANAWAZA JEMA
KISA CHENYE MAFUNZO(VOL 17)
Kulikuwa n mkutano mmoja mkubwa sana uliohusisha viongozi mbali mbali wa nchi za Afrika,Asia na Ulaya.Kikao kilfanyika kwenye hoteli moja nchini Misri yenye ukumbi maalumu wa mikutano,Katika chumba cha mkutano kulikuwa na meza kubwa sana na ndefu ambako wajumbe walikaa kwa kuizunguka meza hiyo.
Kwenye kile kikao agenda ilikuwa na kupanda kwa gharama za mafuta na athari yake kwenye uchumi wa dunia.
Kikao kilichukua takriban siku tano,wajumbe wa kikao kutoka nchi mbali mbali walikuwa wakichangia agenda iliyopo mezani huku mjumbe mmoja wa kutoka nchi flani(yoyote unayoifirikia)
Ilipofika siku ya nne kabla ya kufunga kikao mjumbe mmoja akaamua wa kikao akasema kwa kuwa kuna mwezetu mmoja hajachangia toka kikao kianze siku ya kwanza mpka leo siku ya nne basi tumpe nafasi ya kuchabgia muda huu maana atakuwa alikuwa akifikaria kwa undani sana kuhusu swala hili.
Alipokaribishwa na kuanza kuzungumza alichokisema kiliwashangaza watu na hawakuamini kama kweli siku zote zile anaweza kuja na mazwazo kama yale...."Kwa kweli hamkokosea mimi nimekuwa kwenye dimbwi la mawazo toka siku ya kwanza kuingia humu ndani kwani nimekuwa nikijiuliza ule mlango tunao ingilia ni mdogo sana lakini hii meza kubwa sana hivyo najiuliza hii meza iliingiaje humu ndani?kwa kweli mpka sasa bado najiuliza...."
Kisha akaa chini
FUNZO:SI KILA UNAEMUONA YUPO KWENYE DIMBWI LA FIKRA BASI ANAMAWAZO MAZURI WENGINE HUWAZA VITU VYA KIJINGA KABISA
0 comments :
Post a Comment