Na Stratton Hatfield.
Katika kujiokoa kwenye hatari yeyote ile si tu watu ambao wanaweza
kupata wazo la ajabu la kutenda ilimradi tu kuepukana na mauti, fisi
mmoja aliyekuwa katika lishe yake alijikuta katika wakati mgumu baada ya
kulazimika kujificha kwenye tumbo la mzogo wa tembo ili kumkwepa simba
dume aliyemvamia ghafla.
Fisi huyo aliyaona mauti yaleeeeee, lakini aliona ni heri kukaa ndani ya tumbo la tembo kulikoni kuliwa na simba. picha zifuatazo zinaonyesha namna fisi huyo alivyojificha na baadae kufanikiwa kukimbia baada ya kupata upenyo.
Tukio hilo halijatokea mbali bali ni kule Masai Mara, pata uhondo huo.
0 comments :
Post a Comment