KISA CHENYE MAFUNZO(VOL 23)
Mdada mmoja aitwae Toza alkuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu flani katika jiji la Dar es salaam.Maadili yake hayakufanana na elimu yake,kwani mavazi yake yalikuwa tight pamoja na vimini.Pia alikuwa mwingi wa dharau hasa kwa wale aliowazidi umri.Alikuwa amepanga kwenye hosteli moja hivi katika jiji la Dar es salaam ambako alijikuta chumba kimoja na binti wa ngazi ya cheti huku yeye akiwa ni mwanafunzi wa shahada ya kwanza.
Waliishi kwa muda mrefu sana pamoja huku bini wa ngazi ya cheti akivumilia dharau nzito zilikuwa zikitoka kwa Toza.Siku yule binti wa ngazi ya cheti aliangusha kadi iliyosomeka kama ANGAZA huku ikionyesha yule binti kuwa ni muathirika.Toza alilama sana na kumtolea maneno ya kashfa na ya kiunyanyapaaji kwa yule binti kisha akasema siwezi tena kukaa chumba kimoja na wewe usije niambukiza maradhi maana wewe ni marehemu mtarajiwa.
Toza alihama chumba na kujiunga na mabest zake waliokuwa wawili kwenye chumba cha jirani.
Baada ya wiki moja kupita siku ya jumamosi Toza akiwa amevaa kimini na blauzi iliyoacha mgongo wake wazi akiwa na marafiki zake walikatiza maeneo ya ilala mida ya asubuhi na kung'atwa na MBU wa DENGUE pasina yeye kufahamu.Ilikuwa bahati mbaya kwake kwani ni yeye peke yake ndiye aliyeng'atwa na mbu huyo kwa sababu sehemu kubwa ya mwili wake ulikuwa wazi.
Siku tatu baadae akaanza kuhisi maumivu ya kichwa makali sana hasa maeno karibu na macho pia akaanza kupatwa na dalili zingine za malaria.Kama ilivyo desturi ya watanzania wengi Toza hakwenda kupima bali alinunua declophenac ili atulize maumive kisha ameze dawa za malaria kama hali itakuwa bado.
Alipomeza declophenac hali ikabadilika na kuanza kuhisi maumivu kwenye sehemu za maungo ya mguu na mikono,Alila kwa shida huku akijipa moyo kuwa akiamka hali itakuwa shwari.Haikuchukua hata masaa tisa Toza akaanza kuvuja damu sehemu zote za matundu ya mwili na kufanya wenzake wamuogope hata kumshika.Waliita ambulance ikaja kumbeba huku kila mtu hataki hata kumgusa ispokuwa wahudumu tu wa ambulance .Madaktari walimfanyia vipimo na kugundua kuwa ni HOMA YA NDENGU.Daktari akasema apelekwe kwenye chumba cha wagonjwa wa HOMA YA DENGUE lakini kwa bahati mbaya walikuta tayari Toza ameshafariki duniaa.
FUNZO:kuwa na UKIMWI haimaanishi utakuwa wa kwanza kufa
Usinyanyapae wagonjwa wa Ugonjwa wowote
HEBU WEKA NA NYINGINE HAPO CHINI

0 comments :
Post a Comment