Watu wawili wamejeruhiwa katika mlipuko uliotokea mjini Mombasa pwani ya Kenya.
Miongoni mwa wawili hao ni afisa wa polisi aliyekimbizwa katika hospitali ya mkoa kupokea matibabu.
Shambulio hilo litokea wakati maafisa wa
polisi walimkamata mshukiwa wa ugaidi, na hapo pakatokea mtu wa pili
aliyewarushia guruneti katika jitihada ya kumuokoa mshukiwa
aliyekamatwa.
Mbunge wa Mvita kutoka eneo hilo, Abdulswamad
Sharrif ambaye ni miongoni mwa viongozi waliofika katika eneo hilo punde
baada ya mlipuko huo, amelaumu udhaifu katika idara ya ujasusi Kenya
kwa kutoweza kutambua mipango ya mashambulio kama hayo kabla ya
yafanyike, ili kuweza kuyatibua.
Akizungumza na BBC Abdulswamad amesema, 'Ni lazima tuweze kukubali kasoro iko wapi, ili tuweze kujua suluhisho litakuja vipi'.
Shabulio hilo limetokea wakati usalama
umeimarishwa nchini Kenya kutokana na tisho la kutokea shambulio la
kigaidi dhidi ya maeneo ya umma.
Katika siku za hivi karibuni Kenya imekuwa
ikikabiliwa na mashambulio kadhaa katika maeneo mbali mbali nchini
ukiwemo mji huo wa Mombasa na Nairobi, yaliosababisha vifo vya watu
kadhaa na wengine wengi kujeruhiwa.
Ni hivi juzi tu watu 10 waliuawa huku zaidi ya
hamsini walijeruhiwa katika milipuko miwili iliotokea katika Soko kubwa
la nguo la Gikomba katika mji mkuu Nairobi
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment