-->

HATIMAE VAN GAAL ASAINISHWA MKATABA WA MIAKA MITATU NA KUWA KOCHA MPYA YA MAN UNITED

Van Gaal
Louis van Gaal ametangazwa kuwa kocha mpya wa Manchester United, huku aliyekuwa kocha wa muda Ryan Giggs akifanywa kuwa msaidizi wake.
Raiya huyo wa Uholanzi, ametia saini mkataba wa miaka mitatu, na atachukua usukani wa timu hiyo baada ya kuiongoza timu ya taifa ya Netherlands katika kombe la dunia litakalofanyika nchini Brazil.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 62 amewahi kushinda mataji na vilabu vya Ajax, Barcelona na Bayern Munich.
Manchester United ilimfuta kazi David Moyes mwezi Aprili, miezi 10 tu baada ya kuchukua usukani baada ya kustaafu kwa Alex Fergurson, aliyekuwa mkufunzi wa timu hiyo kwa miaka 26.

Ufanisi wa Van Gaal

Mataji ya kitaifa:
Ajax (1993-94, 1994-95, 1995-96),
Barcelona (1997-98, 1998-99),
Bayern Munich (2009-10)Klabu bingwa ulaya:
Ajax (1994-95)Kombe la Uefa:
Ajax (1991-92)
Gigs aliye na umri wa miaka 40 alichukua usukani kama mkufunzi wa muda katika mechi nne za mwisho wa msimu uliopita.
Alikutana na Van Gaal nchini Netherlands juma lililopita ili kuzungumza kuhusu hatima yake katika klabu hiyo, kama mmoja kati ya wakufunzi na wakati huo huo akiwa mchezaji.
United walimaliza wa saba katika ligi ya premier, baada ya waliokuwa mabingwa watetezi kushindwa na Manchester City, Liverpool na Chelsea.
Walishindwa kufuzu kucheza mechi ya vilabu bingwa wa Uropa kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1995-96, na hawatacheza mechi zozote za kiropa kwa ujumla kwa mara ya kwanza kwa miaka 26 iliyopita.
Mchezaji mkongwe wa klabu hiyo Giggs, meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti na meneja wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp walikuwa wamehusishwa na kazi hiyo, lakini Van Gaal ndiye aliyechaguliwa ili kuiongoza timu hiyo kurejea kileleni mwa ligi za premier na michezo ya Uropa
Kocha huyo mpya anatarajiwa kupewa pesa nyingi ili kuwasajili wachezaji wapya
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment