-->

GAURDIOLA ATWAA KOMBE LA DFP POKAL KWA KUMCHA DORTMUND 2-0

406919_heroa 
PEP Guardiola amekiri kuwa haikuwa kazi nyepesi kurithi mikoba ya Jupp Heynckes katika klabu ya Bayern Munich msimu huu baada ya kocha huyo kushinda makombe matatu ikiwemo la nyumbani na Ulaya.
Guardiola aliwashuhudia vijana wake wakiifunga Borussia Dortmund mabao 2-0 na kubeba kombe la DFB-Pokal siku ya jumamosi.
Mbali na kombe hilo, kocha huyo pia alitwaa ubingwa wa Bundesliga katika msimu wake huu wa kwanza klabuni hapo.
Hata hivyo mafanikio hayo yamezibwa na kufanya vibaya katika michuano ya UEFA ambapo walitolewa hatua ya nusu fainali kwa kipigo cha mbwa mwizi dhidi ya Real Madrid.
“Ni mwaka wangu wa tano nikiwa mkufunzi wa soka , mwaka wangu wa sita nikiwa kocha mkuu”. Guardiola aliwaambia waandishi wa habari.
“Mwaka mmoja nilikuwa naifundisha Barcelona B. Baada ya miaka minne nilikuwa kocha mkuu wa Barcelona. Kipindi hiki kilikuwa muhimu kwangu na nilikabiliana na changamoto nyingi katika maisha yangu ya ukocha”.
“Hapa Ujerumani sijafanikiwa na ndio maana kila wakati nawahamasisha wachezaji wangu. Baada ya Bayern kushinda mataji matatu chini ya Jupp Heynckes, haikuwa rahisi kwangu”.
“Bado sijafanikiwa kuiweka timu nipendavyo mimi. Kuna kazi kubwa ya kufanya, lakini tunajivunia kwa makombe haya”.
Pia Guardiola ameisifu bodi ya Bayern kwa kumpa kibarua na kusema anataka kuwaletea mafanikio zaidi.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment