MTANZANIA
Adam Nditi jana alicheza kwa dakika zote 90 wakati Chelsea ikiichapa
Manchester United mabao 2-1 na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vijana
chini ya umri wa miaka 21 England Uwanja wa Old Trafford.
Nditi
na mchezaji mwenake wa Chelsea, Swift walionyeshwa kadi za njano katika
mcheo huo uliohudhuriwa na kocha wa muda wa United, Ryan Giggs na
msaidizi wake, Paul Scholes sawa na Pearson na Ekangamene kwa upande wa
Mashetani Wekundu.
Washindi:
Adam Nditi mbele ya bango kulia akiwa na wachezaji wa Chelsea
wakisherehekea taji lao la U-21 la ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya
kuifunga Manchester United mabao 2-1 katika fainali jana Uwanja wa Old
Trafford
Huruma: Wachezaji wa Man United wakiwa wamejiinamia baada ya Chelsea kufanya yao Old Trafford
Kiboko yao: Lewis Baker akisherehekea boa la ushindi lililoipa ubingwa Chelsea jana
Walimshuhudia Nditi: Paul Scholes (kushoto) na Ryan Giggs walikuwepo Uwanja wa Old Trafford jana
Mtanzania Ulaya: Kiungo Adam Nditi wa Chelsea kushoto akimkabili Varela wa Man United na kulia na mchezaji mwenzake, Nathan Ake.
Katika mechi hiyo tamu ya fainali, United walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 12 kupitia kwa Lawrence, kabla ya Charly Musonda kuisawazishia The Blues dakika ya 21 na Lewis Baker kufunga la ushindi dakika ya 78.
Katika mechi hiyo tamu ya fainali, United walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 12 kupitia kwa Lawrence, kabla ya Charly Musonda kuisawazishia The Blues dakika ya 21 na Lewis Baker kufunga la ushindi dakika ya 78.
Kikosi
cha Manchester United kilikuwa: Amos, Varela, McNair, M Keane,
James/Blackett dk81, Janko, Ekangamene, Pearson, A Pereira,
Lawrence/Harrop dk84 na Wilson/Weir dk67.
Chelsea:
Blackman, Ssewankambo, Aina, Christensen, Nditi, Loftus-Cheek/Palmer
dk77, Baker, Ake, Swift, Feruz na C Musonda/Colkett dk85.
0 comments :
Post a Comment