-->

KISA CHENYE MAFUNZO(VOL 18)

KISA CHENYE MAFUNZO(VOL 18)
Kijana mmoja machachali aitwae Zomo ambae hakubahatika kuoa katika umri wake wa miaka 29 alikuwa akitembea na wanawake pasina kuwaoa.Kijana huyo ambae alikuwa mkazi wa kijiji cha mkalabanzi mkoani Samizu katika ya nchi ya Dhanio alikuwa na mahusiano na msichana mmoja ambae alikuwa yuko mbali na kijiji chao kilipo.
Katika kijiji cha Michaze kilichopo karibu na kijiji cha Mkalabanzi kulitokea tukio la wizi katika mida ya usiku wakati wenye wako ndani wakitizama tv huku nje vibaka walipitia nguo zilizo anikwa pamoja na kutoboa madirisha na kuchukua baadhi ya vitu vilivyopitishiwa kwenye dirisha.Tukio hilo lili wakera sana wakazi wa kijiji hicho kiasi cha kujiapiza kwamba siku tukimkamata mwizi atakoma.
Usiku mmoja tulivu kijana Zomo kama walivyo vijana wengi wakisasa alifunga safari mpaka nyumbani kwa yule binti na kuanza kutizama huku na kule labda atatoka nje lakini haikuwa hivyo.Baada ya muda mrefu kupita kijana yule akalazimika kwenda kuichungulia dirishani ili kama atamuona aweze kumpa sign ya kutoka nje ili aongee nae.
Kipindi anachungulia dirishani mmoja wa nyumba ya jirani alimuona mtu huyo akiwa na macho ya wasi wasi mithili ya paka mwizi.Hakufanya ajizi akawapigia simu wenye nyumba kwa siri na kuwaambia watoke na siraha kwani kuna kibaka anataka kuiba na yupo dirishani.
Zomo alipoona hamuoni yule msichana hata kwa pale dirishani ndipo alipowasha tochi ya simu yake ili amulike vizuri.Ghafla akavamiwa na kundi lenye siraha na kuanza kupigwa vikali.Mazingira yalionyesha kama vile Zomo ni mwizi hivyo hakuna aliyehoji bali ni kutupa vitofa na kumkatakata kwa mapanga mpaka akakaribia kufa.
Ili kuonyesha hasira zao wananchi walitoa mafuta ya taa na kumwagia kisha kumchoma moto.ndani ya lisaa limoja kijana Zomo akwa amepoteza maisha.
Asubuhi kulipokucha yule mdada aliyekuwa akitembea na Zomo alishanga kukuta ile maiti iliyowaka moto ni ya yule awala yake.Alilia pasina kujizua na kutamka mmemua bure huyu sio mwizi,ni boyfriend wangu na alikuja kunifuata mimi.Na ilipotizamwa simu ya yule binti ni kweli ikaonekana kwamba meseji ikisema NIPO DIRISHANI KWENU KWA HAPA NJE, WEWE UKO WAPI??UKIONA MWANGA WA TOCHI UJUE NI MIMI...................
I AM CURIOUS WAITING YOU.........................................
Hatimae kila mtu alijua kwamba wamemuua mtu sie na huo ndio ukawa mwisho wa kijana Zomo.
FUNZO:msikae na watoto wa watu vichochoroni
usimpige mtu hovyo pasina kuwa na ushahidi
kama unampenda muoe acha kumdanganya
HEBU WEKA NA MAFUZNO MENGINE

picha hii imetoka maktaba ya kalulunga blog na wala si ya kisa hiki
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment