Winga wa kimataifa wa Wales na klabu ya Manchester United Ryan Giggs ametangaza kustaafu.
Giggs
ambaye alianza kuichezea timu ya watoto ya Manchester United mnamo
mwaka 1991, amestaafu soka baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 23
mpaka sasa huku akifanikiwa kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi
katika klabu yake ya Manchester United – akiichezea mara 963.
Giggs
anastaafu akiwa ndio mwanasoka ambaye kashinda makombe mengi zaidi –
makombe 13 ya premier league, FA Cup 4, Capital One 4, mawili ya kombe
la klabu bingwa ya ulaya na 2 klabu bingwa ya dunia.
Giggs
pia ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa ligi mara mbili mwaka
1992 na 1993, pia alishinda tuzo hiyo kutoka kwa klabu ya Manchester
United mwaka 1991 na 1992.
Mnamo
mwaka 2009 alishinda tuzo ya BBC Sports Personality of the Year na paia
akashinda PFA Player of the Year award. Ametajwa kuwa mchezaji bora
mwaka wa ligi kwa mara 6.
Gigs
alicheza mechi yake ya mwisho na United kwenye mchezo dhidi ya Hull
City mwanzoni mwa mwezi huu ambapo United walishinda 3-1. Alishikilia
uongozi wa benchi la ufundi kwa muda baada ya David Moyes kufukuzwa, na
sasa atakuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo nchini ya Louis Van Gaal.
0 comments :
Post a Comment