-->

HIKI NDICHO ALICHOANDIKA SAMSON MWIGAMBA KWENYE FACEBOOK KUHUSU ACT-TANZANIA

 
ACT - TANZANIA! TAIFA KWANZA!


Napenda kuchukua fursa hii kuwataarifu wana ACT-TANZANIA nchi nzima kwamba chama chenu kitakabidhiwa Cheti cha Usajili wa Kudumu na Msajili wa Vyama vya Siasa Mei 5, 2014 kama ilivyopangwa. Na kwa hiyo natangaza kwamba Birth Day ya ACT - TANZANIA ama ACT DAY itakuwa ni Mei 5 ya kila mwaka.
Naomba tuwe na subira mpaka hapo kamati ya muda ya kitaifa itakapoketi siku chache zijazo kwa ajili ya kupanga ratiba na program ya chama kuanzia sasa mpaka Dec. 2014 ikijumuisha uchaguzi mkuu wa kwanza wa chama, uzundizuzi rasmi wa chama na maandalizi ya ushiriki wetu kwenye chaguzi za kiserikali zilizo mbele yetu ikiwa ni pamoja na uchaguzi wowote mdogo utakaotokea hivi karibuni.
Kazi kubwa tuliyonayo kwa sasa ni kukieneza chama mpaka ngazi za chini kabisa. Tunafanya kila juhudi kuchapisha kadi mpya na bendera mpya kwa ajili ya kazi hiyo. Wakati zinasubiriwa hizo, endeleeni kutumia hizo zilizopo na pengine kutumia madaftari kuorodhesha wanachama wenu kadi zitakapokuja mtawapa. Mkoa wowote ambao tayari una wanachama wa kutosha lakini hawajawa na viongozi wa muda (waratibu) wawasiliane na Naibu Katibu Mkuu Bara (Leopold Mahona - 0758409670 / 0787457970) ama Katibu Mwenezi Taifa (Masaga Mohamed Masaga - 0718388888 / 0766845424) kwa ajili ya maelekezo ya namna ya kuchagua waratibu wa muda. Rasimu ya mwisho ya Katiba inakamilishwa, ikishakuwa tayari itawasilishwa kwenye kamati ya taifa na baadaye kwa wadau wote ili mpate kutoa maoni yenu kabla ya kuja kupitishwa rasmi kwenye mkutano mkuu maalum.
Nawatakia heri na Baraka za Mwenyezi Mungu Subh-a-annah wat-a-allah katika ujenzi wa chama mbadala kwa ajili ya TANZANIA TUITAKAYO!!!
MABADILIKO NA UWAZI! CHUKUA HATUA!
Maingu Samson Mwigamba,
Katibu Mkuu.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment