Demba Ba mchezaji wa Timu ya Soka ya Chelsea
katika ligi ya Premier nchini nchini Uingereza amefadhili kikamilifu
ujenzi wa msikiti katika nchi yake asili, Senegal.
Demba Ba mchezaji mashuhuri wa Chelsea amegharamia ujenzi wa msikiti
uliopewa jina la ‘Masjid Nasrullah’ katika eneo la Fouta kijiji cha
Doondu kaskazini mwa Senegal.Vyombo vya habari Senegal vimeripoti kuhusu mchango wake huo kabla ya kufunguliwa msikiti huo adhimu katika kipindi cha siku chache zijazo. Demba Ba ni mchezaji mashuhuri Mwislamu nchini Uingereza ambaye husherehekea mabao aliyofunga kwa kusujudu katika ardhi na kumshukuru Mola. Mchezaji huyo wa Chelsea anasema alilelewa katika familia yenye kufuata misingi ya dini ya Kiislamu.
“Kuwa Mwislamu ni muhimu kwangu mimi zaidi ya kuwa mchezaji. Mwislamu mzuri huwa na shakhsia bora na hivyo mimi hujaribu kuwa mtu mzuri,” alisema wakati akihojiwa na gazeti la Independent mwaka jana. Mchezaji huyo Mwafrika anasema yeye husali mara tano kwa siku, havuti sigara wala hanywi pombe.
Demba Ba ambaye asa ni raia wa Ufaransa ana asili ya Senegal, nchi ya Magharibi mwa Afrika ambayo asilimia 90 ya watu wake ni Waislamu.
0 comments :
Post a Comment