Tangu
mwaka 2012 zaidi ya watoto 154 wamezaliwa na wanawake walio juu ya umri
wa miaka 50. Miongoni mwao, wamo waliotokana na teknolojia ya
upandikizaji.
Pamoja
na madaktari kuonya kuwa kuzaa katika umri mkubwa kunahatarisha maisha
ya mama na mtoto, wanawake hasa matajiri wamekuwa wakizaa katika umri
mkubwa. Wilayani Handeni Mkoa wa Tanga, Mwajuma Seif (50) aliweka rekodi
ya kujifungua watoto mapacha katika umri huo.
Lakini
Mwajuma ana kingine cha ziada tofauti na wanawake wengi wanaozaa katika
umri huo; alizaa kwa njia ya kawaida na si kwa teknolojia ya
upandikizaji.
Tofauti nyingine ya mwanamke huyo si kwamba alizaa katika umri huo kwa kuwa hakuwa na mtoto; ujauzito huo ulikuwa ni wa 13.
Daktari
anayemwangalia Mwajuma, Elinisa Mushi anasimulia mkasa wa mwanamke huyo
akisema pamoja na umri, kingine kilichomshangaza ni mtoto wa ajabu
aliyemzaa.
Anaeleza
kuwa walimpokea Mwajuma, ambaye ni mkazi wa Kata ya Sindeni zaidi ya
mwezi mmoja uliopita akiwa na ujauzito, lakini walishangazwa na tumbo la
mama huyo kwani lilikuwa kubwa sana kiasi cha kuhisi kulikuwa na tatizo
fulani. Ndipo walipoamua kuanza kumfanyia uchunguzi.
Baada
ya kupima ujauzito huo kwa kutumia mashine ya ultra sound (kamera ya
mionzi), waliona ni kweli tumboni kuna watoto wenye maumbo yasiyoeleweka
hivyo walitaka kumsafirisha kumpeleka Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo
lakini walishindwa kutokana na hali yake.
Anasema
baada ya kugundua kuwa hawataweza kumsafirisha kutokana na hali yake,
ilibidi wamuweke katika ulisimamizi maalumu hadi siku ya kujifungua.
Alijifungua kwa njia ya upasuaji.
Katika upasuaji, madaktari walimtoa mtoto wa kwanza mwenye umbo la ajabu akiwa na kilo sita na wa pili akiwa na kilo 1.5.
Anafafanua
kuwa mtoto alipotolewa tumboni ingawa hakuwa wa kawaida, alikuwa
anapumua. Baada ya muda alianza kutoka maji na saa moja baadaye
alifariki dunia. Mtoto mwingine aliishi kwa siku moja na akafariki.
“Alikuwa
na kilo sita pia alikuwa amevimba sana. Huu ni uzito mkubwa sana kwa
mtoto. Baada ya muda mfupi alianza kutoka maji hadi mwili ukapungua
kiasi na baadaye alifariki. Mwenzie aliendelea kuishi kwa saa 24,”
anasema Dk Mushi.
Mtoto
huyo alizaliwa akiwa na miguu yote miwili, lakini iliyoungana na kichwa
chenye mdomo na masikio yanayoonekana kwa mbali. Hana kiuno wala
mikono.
Source: Mwananchi
0 comments :
Post a Comment