-->

FREEMAN MBOWE AVUNJA UKIMYA,AZUNGUMZIA KASHFA YA GARI LAKE KUHUSISHWA NA UGAIDI

FREEMAN MBOWE AZUNGUMZIA SAKATA LA GAR YAKE KUKAMATWA NCHINI KENYA
kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni,mbunge wa Hai na mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe amevunja ukimya na kuamua kuzungumzia sakata la gar yake kukamatwa nchini Kenya.
Hivi sasa nchini kenya kumetanda hofu kubwa ya mashambulizi ya Al-shababy,Al-shababy wameshafanya mashambulio kadhaa ya kigaidi nchini humo na wameahidi kuendelea na mashambulio hayo mpaka pale kenya itakapoondoa majeshi yake nchini Somalia
Kufuatia tishio hilo la ugaidi,polisi wa kenya wamekuwa wakifanya doria usiku na mchana kuhakikisha wanadhibiti jaribio lolote la Al-shababy,polisi hao wamekuwa makini sana na watu woote wanaoingia na kutoka nchini humo
April 26 mwaka huu,mh Mbowe alisafili kwa njia ya barabara akielekea nchini kenya huku akiwa ameambatana na mh Ezekiel Wenje,baadae aliliacha gar hilo na kupanda ndege mpaka Nairobi,polisi walilitilia shaka gar hilo lilikuwa na namba mbili STK, KUB na kumuamuru dereva wa gar hilo kulipeleka kituoni kwa ajili ya mahojiano
Baada ya kufika kituoni dereva aliwaambia polisi kuwa gar hilo ni la mh Mbowe ambae alikuwa nchini humo,baada ya kusikia maelezo yale wakafanya uchunguzi ili kubaini kama kweli gari hilo ni la mh Mbowe,walipohakikisha kuwa ni la mh Mbowe wakamuachia huru dereva hyo lakini wakaendelea kulishikilia gar hilo
Baada ya mbowe kupatikana alifanya mazungumzo na polisi hao kwa muda mfup sana,polisi hao wakamshangaa Mbowe na kumuuliza kwanini kiongozi mkubwa kama yeye anatembea bila ulinzi,mbowe akawajibu kwa kuwaambia kuwa hilo jambo ni lakawaida sana nchini Tanzania,baada ya mazungumzo hayo mbowe akaruhusiwa kuondoka na gar lake,
Polisi wa kenya wamesema hakuna uhusiano wowote kati ya gar hilo na ugaidi
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment