Simba wakianza kujipanga kwaajili ya mashambulizi katika kundi la Nyati 6 walio waona.
Nyati
huyu ndio aliingia katika mtego na kuanza kufukuzwa na Simba. Kwa Mbali
gari la Watalii likija eneo hilo na baada ya muda magari 12 yaliyo na
watalii mbalimbali yalifika katika eneo hilo na kushuhudia mtanange
mkali kati ya Simba na Nyati. Mpigapicha wa Gazeti la Uengereza la Daily
Mail, Scott Macleod alinasa taswira hizi.
Simba wakianza jitihada za kumuangusha Nyati huyo dume bila mafanikio.
Ilikuwa ni vita ambayo haikuruhusu mtoto kutumwa maji dukani.
Ubabe wa Simba ilizidi kuongezeka kwa wafalme hao wa Pori kujaribu kumuua mmoja wa wanyama wakubwa 5 Porini. The Big 5 Animal
Watalii
walikata kiu yao vya kutosha maana moja ya vitu vinavyowavutia watalii
ni kumuona Simba au Chui akiwa mawandoni. Lakini hakika kwa Hifadhi za
Tanzania hili linawezekana na watalii karibuni mjionee haya.
Mziki uliendelea ...
Watalii waliongezeka...jitihada za Simba walau kumuangusha Nyati hiyo bila mafanikio.
Simba
hawakuhofua macho wala mingurumo ya magari iliyokuwa imewazunguka
mahali hapo wakati vita yao ya kumla Nyati ikiendelea. Watalii
wakifurahia kivutio hicho ndani ya ardhi ya Tanzania.
Hakika
Nyati ni The Big 5 Animal. Licha ya Simba kuwa wengi lakini walishindwa
kumuangusha Nyati huyu na kujipatia kitoweo. Simba walitawanyika kwenda
kutafuta nguvu zaidi.
0 comments :
Post a Comment