-->

AMRI KIEMBA ASAINI YANGA

clip_image002WAKATI Haruna Niyonziam akiwa amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga, habari zilizotufikia hivi punde zinasema kiungo wa Simba, Amri Kiemba amesajiliwa na Yanga tayari kwa kuitumikia timu hiyo kwa msimu ujao.
Akizungumza na mtandao huu, mtu mmoja kutoka kamati ya usajili ya Yanga, amesema Kiemba amesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili ili kuongoza nguvu katika safu ya usajili ya Yanga.
Mtandao huu unaahidi kuwasiliana na Kiemba muda mfupi atakapotoka mazoezini katika kambi ya Taifa Stars kujiandaa na mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2014.
Atakapotoka mazoezini mtandao huu utawasiliana naye kiungo huyo ili aweze kueleza ukweli juu ya usajili wake kwa Yanga.
Kiemba aliwahi kuichezea Yanga miaka ya nyuma kabla ya kutimka katika timu hiyo.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment