KUSTAAFU SIR ALEX FERGUSON: NINI WANASEMA??
Jumatano, 08 Mei 2013 16:58
>>CRISTIANO RONALDO: “ASANTE SANA KWA KILA KITU, BOSI!”
>>SEPP BLATTER: “NI NGULI!”
>>PAUL INCE: “HATUWEZI TENA KUONA MTU AINA HII!”
>>CHELSEA: “KILA LA HERI SIR ALEX FERGUSON! ALIKUWA MPINZANI SAFI KWA MIAKA 26!”
DUNIA YA SOKA leo ilipata mtikisiko pale Meneja waManchester
United, Sir Alex Ferguson, alipotangaza kustaafu mwishoni mwa Msimu huu
baada ya kuwa hapo kwa Miaka 26 na kutwaa Mataji ya Ubingwa 13.
WADAU WENGI WALIIBUKA NA KUTOA MAONI YAO KAMA IFUATAVYO:
-Michael Owen, Mchezaji wa zamani wa Man United na England: “Ukisoma rekodi yake ya Umeneja utashtuka!”
-Mchezaji wa zamani wa Man United, Paddy Crerand: “Mungu amsaidie Mtu atakaemrithi kwani viwango alivyoviweka ni vya juu mno!”
-Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron: “Ni Mtu wa ajabu! Natumai kustaafu kwake kutaisaidia Timu yangu [Aston Villa]!!”
-Rais
wa FIFA, Sepp Blatter: “Mafanikio yake kwenye Gemu yanamweka, bila
shaka, kuwa mmoja wa Manguli. Nilipata heshima kubwa kumpa Tuzo Mwaka
2011 kwenye Hafla ya Ballon D'Or. Uwezo wake wa kukaa muda mrefu unaweza
kufikiwa?”
-Rais wa UEFA, Michel Platini: “Yeye ni
Mtu mwenye kuona mbali. Ametoa mchango mkubwa kwa Soka, si Scotland na
England tu, bali Ulaya yote na mbali kote.”
-Mkurugenzi Mtendaji wa Man United,
David Gill: “Alichoifanyia Klabu hii na kwa Soka kwa ujumla
hakutasahauliwa milele. Nimepata mafunzo mengi kwa kufanya nae kazi na
ni heshima kubwa kwangu kumuita ni Rafiki yangu.”
-Nahodha wa zamani wa England na
Mchezaji wa Man United, Paul Ince: “Hutaweza tena kumuona Mtu wa aina
hii tena. Viwango vyake vilikuwa vya juu. Alikuwa akitaka Watu wajitume.
Ndio, tulikuwa na migongano yetu. Lakini alinichukulia mimi kama
Mwanawe. ”
-Kiungo wa zamani wa Man United, Lou Macari: “Je huyo anaekuja kumrithi anaweza kufanya alichofanya Sir Alex? Ni ngumu!”
-Mchezaji wa Real Madrid aliewahi kuwa Man United, Cristiano Ronaldo: “Asante sana kwa kila kitu, Bosi!”
-Rio Ferdinand, Beki wa Man United: “Bosi anatetea kila Mchezaji kwa kila kitu na ndio maana Wacheza wote wanamuheshimu sana!”
-Nayo Klabu ya Chelsea ilituma Ujumbe
kwenye Twitter: “Wote hapa Chelsea tunamtakia kila la heri Sir Alex
Ferguson kwa kustaafu. Alikuwa Mpinzani safi kwa Miaka 26!”
-Kipa wa zamani wa Man United, Peter
Schmeichel : “Hili limekuja kama Bomu. Nimehuzunika na kuvunjwa moyo.
Nilitegemea atakuwepo kwa Miaka kadhaa!!”
-Meneja wa Celtic, Neil Lennon: “Gemu haitakuwa kama ilivyokuwa bila Sir Alex Ferguson!”
credit to sokainbongo
0 comments :
Post a Comment