Hapo jana katika ukumbi wa mambo club uliopo maendeo ya Kihonda magorofani,Wanachama wa CCM wa tawi la chuo Kikuu Cha Waislam Morogoro walikutana kwenye ukumbi huo wa mambo club ili kjadili mambo mbali mbali ya maendeleo ya chama pamoja na taifa kwa ujumla.
Kikao hicho kiliudhuriwa na watu wa rika mbali mbali vijana pamoja na wazee ambao ni wanachama halisi wa chama cha CCM pamoja na viongozi mbali mbali wa CCM na taifa kwa ujumla kam naibu Meya wa mkoa wa Morogoro bibi Lidya,pia alikuwepo diwani wa kata ya Kihonda magorofani afahamikae kama mama Baro,Pia alikuwepo mwenyekiti wa mtaa mama Mwemba.Katika kikao hicho cha Tawi mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Tandaimba ambae ni wakili wa kujitegemea akiwa shahada mbili,pia ni mlezi wa tawi la CCM katika chuo kikuu cha Waislam Morogoro ndugu Juma Abdallah Njwayo.
Katika hotuba yake mheshimiwa Juma Abdallah Njwayo aliwataka wananachama wa tawi hilo kujitahidi kuipata elimu kadri wawezavyo kwani hiyo ni nguzo katika utendaji wa kila jambo.Pia aliwataka wanachama kuwa waelimishaji kwa wananchi hubabaishwa na siasa nyepesi kama vile CCM imeshindwa kutatua tatizo la ajira,Amesema swala la ajira n swala la dunia nzima huku akitoa mfano wa kipindi cha uchaguzi nchini Ufaransa na Marekani kwani wagombea walisikika wakinadi kuleta ajira kwa wananchi wao hivyo hiyo ni ishara kwamba ajira ni tatizo la dunia nzima na CCM inajitahidi kutatua tatizo kadri iwezavyo.
Katika maelezo yake mengine ndugu Juma Abdallah Njwayo amesifu uanzishwaji wa shule za kata kwani zimekuwa suluhisho la kuwa na idadi ya wanafunzi wachache katika elimu ya sekondari tofauti na hapo awali.
Pia ndugu mbunge aliahidi kuchangia laki tano katika mchango wa mahafali na kuahidi kupitisha arambee kwa wenzake ili ipatikane pesa nyingine ili kufanikisha mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa mwaka wa tatu ambao ni wanachama wa chama hicho cha CCM.
Ama nduugu mbunge hakusita kuhimiza swala la upatikanaji wa ofisi maalum kwa ajili ya Tawi hilo la wanafunzi wa chuo kikuu cha Morogoro na kuahidi kuchangia kodi ya miezi mitano ya kuanzia na kusema itakapoisha atafahamishwa na kuendelea na zoezi hilo ili kulifanya tawi hilo imara na lenye nguvu ambalo litatoa watu ambao watakuja kushika madaraka katika ngazi za juu kwa hapo baadae.
Katika kuitimisha kikao kulikuwa na zoezi la utoaji kadi ambao kwa wanachma mpya 15
0 comments :
Post a Comment