Wachezaji wa timu ya Simba Mrisho Ngasa na Shomari kapombe huenda wakapata nafasi ya kwenda kukipiga nchini Uingereza kwani Mmiliki wa timu ya simba Malkia wa nyuki amefanya mazungumzo na mmiliki wa timu ya Sunderland ili waweze kupata nafasi ya wachezaji wake katika timu hiyo ya Sunderland ambayo ipo ligi kuu nchini Uingereza.Malika wa nyuki alikuwepo nchini Uingereza akitizama mechi ya vijana kati ya Newcastle na Sunderland na hivyo alipata nafasi ya kumtupia neno mmiliki huyo wa Sunderland anaeitwa Ellis Short kwamba yeye anavijana wazuri kuliko vijana wa Sunderland,hahah aha ah akacheka kisha akataka kuwajua na kuwapa nafasi ya majaribio kwa vijana hao.Hivyo timu ya Simba fc inasubiriwa kutuma list ya wachezaji chipukizi ambao watakwenda kufanya majaribio nchini Uingereza.
Pia malkia wa nyuki ameeleza kwamba wachezaji hao kama watafuzu majaribio yao basi watapata nafasi ya kucheza ligi ya vijana na jinsi viwango vyao vitakavyokuwa ndivyo watakapofanikiwa kupata nafasi ya kucheza ligi kuu.Wachezaji ambao wamepewa nafasi kubwa kwenda huko ni Mrisho Ngasa na Shomari Kapombe kama ilivyonukuliwa katika mahojiano kati ya malkia wa nyuki na gazeti la CHAMPIONO la tarehe 8-9 la mwezi wa tano mwaka 2013.
Kila la heri kwa timu ya Simba kila la heri kwa Taifa la Tanzania katika maendeleo ya soka hapa nchini.
Picha kwa msaada wa Saleh jembe na Global publishers

0 comments :
Post a Comment