CHUO CHA KIU-DCC KUSIMAMISHWA KUTOA MAFUNZO YA SHAHADA ZA UZAMILI NA UZAMIVU
Kampala International University, Kampasi ya Dar-es-Salaam (KIU-DCC)
kilichopo Gongo la Mboto, Dar-Es-Salaam ni Chuo kilichopewa idhibati na
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). Kufuatia kuendesha mafunzo ya
shahada ya Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) kinyume cha
utaratibu na kutokua na wahadhiri wa kutosha wenye sifa stahili, Tume
katika mkutano wake wa hivi karibuni ulikiamuru Kampala International
University, Kampasi ya Dar-es-Salaam ifuatayo;
1. KIU isimamishe mara moja mafunzo yote ya shahada za juu
(Postgraduate) ikiwa ni pamoja na Shahada za Uzamili (Masters) na
Shahada za Uzamivu (PhD) katika kampasi ya Dar-es-Salaam.
2. KIU ishirikiane na wanafunzi wote iliyowadahili katika programu
zilizotajwa hapo juu waweze kuhamia kwenye vyuo vingine vyenye idhibati
ya kutoa mafunzo hayo.
Tume haitatambua shahada yeyote ya Uzamiili au Uzamivu itakayotolewa na
chuo hicho kwa watakaosoma katika kampasi ya Dar-es-Salaam. Angalizo:
Chuo cha KIU Kampasi ya Dar-es-Salaam kina ithibati na kitaendelea
kutoa mafunzo ya shahada ya kwanza (Bachelors), Diploma au vyeti
zilizopitishwa na TCU kwa mujibu wa Ithibati husika tuu.
Imetolewa na:
Katibu Mtendaji
TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)
source:jamii forum
Home
/
Uncategories
/
TCU WAKIFUNGIA CHUO CHA KAMPALA INTERNATIONAL UNIVERSITY ( KIU ) KWA KUTOKIDHI VIGEZO
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment