Habari zilizotufikia hivi punde kwamba MTWARA PAMENUKA watu wamejifungia ndani na maduka na sehemu nyingine zoote za biashara zimefungwa.Toka asubuhi maduka hayakufunguliwa na sehemu zingine mbali mbali za utoaji huduma za kijamii pia zimekuwa zikikosekana ikiwa ishara ya kuonyesha hasira yao dhidi ya mpango wa kusafishwa gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam.Hali ilibadilika zaidi baada ya kusemekana kwamba kwa mujibu wa lipoti ya waziri wa nishati kwamba gesi hiyo itasafirishwa kuelekea kupitia bomba ambalo litachimbwa na serikali.Hivyo kumekuwa na vurugu kuanzia maeneo ya stendi,Geza,Magomeni na maeneo mengine.Bado haijafahamika kama kuna mtu yoyote ambaye amepoteza maisha kutokana na vurugu hizo bali milio ya risasi pamoja na mabomu yamekuwa yakisika katika maeneo mbali mbali.Pia kuna habari kwamba kuna askari ambae amechomwa mshare(bado haijathibishwa) pia kuna habari nyingine kwamba kuna silaha mbili za polisi zimeporwa na wananchi(Bado haijathibitishwa).kuna habari pia za kuchomwa kwa nyumba ya wageni pamoja na nyumba za viongozi.
ENDELE KUWA NASI ILIUNDELEE KUPATA HABARI YA YANAYOJILI MTWARA
pia unaweza kubofya hapa kwa habari zaidi MTWARAKUMEKUCHA
0 comments :
Post a Comment