-->

MAHAFALI YA VYUO VIKUU CCM MOROGORO YAVUNJA REKODI

Hapo jana tarehe 31 mwezi wa tano mwaka huu 2013 kulikuwa na mahafali yaliyohusisha vyuo vikuu vyote vya mkoani Morogoro kama vile SUA,Mzumbe,Jordan, pamoja na MUM ambao wao ndio walikuwa wenyenyeji wa mahafari.Mgeni rasmi wa mahafali hayo alikuwa ni mheshiwa Mwigulu Nchemba mbunge wa Singida,mwanharakati,msema kweli au mpigania haki ikiwa ni majina ambayo unaweza kumpa kulingana na kazi anazozifanya katika taifa na chama.Mahafari yalihusha pia viongozi wengine kama vile ndugu Abdallah Njayo mbunge wa Tandaimba na mlezi wa tawi la CCM katika chuo kikuu cha waislam Morogoro,Mheshiwa Mtera Mwampamba mgombea wa ubunge kupitia tiketi ya CHADEMA Mbeya ambae alijiunga na CCM na kuamua kuachana na CHADEMA,Chistopher Ndubiagai na wengine kibao.
Ama kabla ya yote mheshiwa Mtela Mwampamba alipata fursa ya kuzungumza na kugusa baadhi ya mashambulizi dhidi ya cham cha mapinduzi kama vile kuwaita mafisadi na kusema kwamba wanaosema hivyo wao pia wanahusika na ishu za ufisadi kama vile Dr. Wilbord Slaa amehusika kufisadi mradi wa KAVIWASU na kuongezea kwamba mbowe ananyumba nje ya nchi huko Dubey,je kamaa nyumba hiyo ukiileta kwenye taswira ya pesa,hiyo haimaanishi kwamba ameweka fedha nje ya nchi?Pia aligusia kwamba Dr Slaa ambae alipinga kuongezwa kwa posho za wabunge swali mbona yeye mshahara wake ni milioni saba?Pia aligusia swala la Mbowe mwenyewe kukili kwamba ametemea ardhini na angani ila hajaona kiongozi bora kama raisi Jakaya Mrisho Kikwete.
Pia mgeni rasmi ambae ni mbunge na pia ni naibu katibu mkuu wa chama cha mapinduzi Tanznia bara ndugu Mwigulu Nchemba alipata nafasi ya kuzungumza na kuwahusia wahitimu yafuatayo;masuala ya ajira,rasilimali pamoja na uzalendo katiak chama na taifa kwa ujumla.alitumia mifano mbali mbali katika kufafanua maeneo hayo..alisema ukienda kila ofisi utakuta kunatatizo la upungufu wa watumishi na huku ukipita kila kona utakuta kuna vijana ambao hawana ajira angawaje wanaelimu ya kutosha.Alitoa wito kwa serikali eidha kuandaa mazingira ya kuwaajili wasomi wanohitmu masomo yao au kuwapa nafasi ya kuendelea na masomo kuliko kuwaacha kukaa mtaani.Pia aligusia swala la uzoefu ambalo limekuwa hitajio kuu katika kila ofisi na wakati hakuna chuo kinachotoa uzoefu bali vyo kazi yao ni kutoa wahitimu thabiti katika fani mbali mbali.Kisha mheshimiwa Mwigulu Nchemba amezungumzia swala la rasilimali kam vile gesi ya mtwala na kusema kwamba kuna watu ambao wanadili zao hivyo wanchochea vurugu kwa maslai binafsi.Kisha alizumzia swala la uzalendo katika nyanja mbali mbali mbali kama vile uhalifu wa kazi za serikali kwa watumishi wa umma kwa lengo la kuikomoa CCM mfano kupeleka pembejeo za mbolea ya vitunguu kwa wakulima wa kahawa au kupandisha bei ya pamba pasina sababu za msingi ili watu fulani wapate jimbo.Katika maeleo mengine aligusia walimu ambao wantumia muda mwingi kuwapotosha watoto kwa kuwasema vibaya CCM na kugeuza darasa ulingo wa siasa kwa dakika zaidi ya 45 au kitendo cha kupandisha viwango vya madaraja ya ufauru na huku  shule za kata hazina walimu,vitabu na maabara,aidha amekemea vitendo hivyo na kuwashauri wanchama wa CCM kuwa  waadilifu katika umma ili waweze kuliendeleza taifa pia aliwaongezea msemo wa kuwajaza nguvu wahitmu kwamba
" LAZIMA UWE NA IMANI NA KILE UNACHOKITEKELEZA"
Zifuatazo ni picha mbali mbali zinazoonyesha matukio yalioyofanyika kwenye sherehe hiyo









MHESHIMIWA MGENI RASMI MWIGULU NCHEMBA AKIAGWA KWA SHANGWE
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment