Hapo jana majira ya asubuhi ililipotiwa kwamba kuna mwanamke amejifungua watoto watano mkoani Songea,Kwa mujibu wa mganga mkuu mfawidhi ,Dk. Benedict Ngaiza alilipoti kutokea kwa tukio hilo katika hospitali ya rufaa Songea ambako mwanamke huyo alijifungua kupitia njia ya operesheni.Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake Dk. Mgonde alifanikisha zoezi hilo la kumzalisha mwanamke huyo ambaye alijifungua watoto watano kuanzia saa 5:15 mpaka saa 5:45 asubuhi.Mwanamke huyo amefahamika kwa jina la Sofia Mgaya mwenye umri wa miaka 28 na pia mwalimu wa shule ya sekondari.Mwanamke huyo amejifungua watoto watano wenye uzito tofauti tofauti,watoto hao wa kwanza ana uzito wa gramu 730,wa pili gramu 810, wa tatu gramu 670, wa nne gramu 820 na wa tano gramu 430.Watoto hao katika kuzaliwa kwao wa kwanza kuzaliwa alikuwa ni wa kike wapili ni wakiume,watatu wakiume,wanne wakiume na wa mwisho ni wakike.Watoto walifankiwa kuzaliwa wakiwa wazima kuhifadhiwa chumba cha watoto ambacho hawajatimiza miezi.
Taarifa za kusikitisha ambazo zimelipotiwa jioni hii ni kwamba watoto hao wote watano wamefariki dunia leo hii na mama yao bado yupo Hospitalini akipata tiba.
Blog hii inatoa pole kwa ndugu,familia,na jamaa wa Zakaria Kiswaga ambae ni mume wa Sofia Mgaya kwa msiba uliowakuta na kuwaombea subra kwenye kipindi hiki kigumu.
0 comments :
Post a Comment