IMETOLEWA 3 AUGUST 2012:UFAFANUZI SWALA LA MRISHO NGASA.
============================== ===============
“We uliona wapi dunia nzima timu inapewa mchezaji kwa mkopo halafu
inamsainisha mkataba? Simba lazima ifike wakati waache kurudia makosa,
haya ndio mambo ya Mbuyu Twite sasa,”alisema kiongozi huyo wa Azam
Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa ya ufafanuzi juu ya sakata la mchezaji Mrisho Ngasa ambalo linaonekanakupotoshwa
1. Azam FC ilitangaza kuwa biashara ya mchezaji Mrisho Ngasa ingefungwa
siku ya Jumatano 1/08/2012 saa sabamchana na ilivitaka vilabu vyenye
interest na mchezaji huyo kufika makao makuu ya Azam FC ofisi ndogo
zilizopokwenye kiwanda cha unga cha Azam-Mzizima zikiwa na pesa taslimu.
Bei ya mauzo iliyopangwa ilikuwa ni Dola50,000. Lakini katika
mawasiliano ya email kwa makatibu wakuu wa Simba na Yanga, Azam FC
iliweka bayana kuwailikuwa tayari kushusha bei ya mauzo na ingemuuza
Ngasa kwa timu ambayo dau lake lingekuwa kubwa zaidi yamwenzake.
Kwa maana hiyo biashara ya mchezaji mrisho ngasa ilifanyika kwa uwazi.
Lengo la Azam FC lilikuwa ni kutoa hakikwa kila klabu yenye uwezo wa
kifedha kuweza kupata huduma ya Ngasa.
Pia tunaomba ifahamike
bayana kuwa mchezaji Mrisho Ngasa alipewa taarifa kuwa anauzwa na
aliombwa asaidiekushawishi klabu anayoitaka ifike kwetu na ofa yake.
Ngasa alitamka bayana kuwa yupo tayari kwenda klabu yoyoteambayo Azam FC
itaona imekidhi mahitaji yake kwa masharti kuwa maslahi yake ya
kimkataba kati yake na Azam FCyazingatiwe.
2. Hadi kufikia
siku ya Jumatano 01/08/2012 saa saba mchana. Ni klabu ya Simba pekee
iliyojibu kwa maandishina kuonesha nia ya kumchukua Ngasa. Yanga wao
hawakuwahi kujibu email, ingawa kwa majibu ya simu Mjumbewao wa Kamati
ya usajili Bw Sefu Magari alitangaza kuwa Ngasa hana thamani ya zaidi ya
milioni 20. Na Yangahaikuwa tayari kuboresha ofa yake.
3.
Muda wa kufungwa kwa biashara ya kumuuza Ngasa ulipofika, ni simba pekee
kupitia kwa makamu Mwenyekitiwake Bw Geofrey Ngange na Mhasibu wake
ndiyo waliofika wakiwa na pesa taslimu shilingi milioni 25.
Yangahawakuonekana na hawakutaka kupokea hata simu walizokuwa wakipigiwa
kuulizwa kama wana interest.
4. Kikao cha dharura cha Azam FC
kilikaa na kuamua kuwa biashara ya kumuuza Ngasa ilishindikana kutokana
nakutokupatikana kwa mnunuzi mwenye dola 50,000. Kwa maana hiyo Azam FC
iliamua kumpeleka Ngasa kwa mkopokwenye klabu iliyofika na kuonesha nia
ya kumhitaji (Simba)
5. Simba walipewa sharti la kuhakikisha
wanamlipa Ngasa mshahara wake kamili (TZsh 2,000,000) pamoja nastahiki
zake nyingine zote za kimkataba
6. Sababu za kumpeleka Ngasa kwa mkopo ni kumuepusha na adhabu ambayo klabu ya Azam FC ingetoa kwaNgasa kama angebaki.
7. Azam FC inapenda kuweka wazi kuwa haijamlazimisha Ngasa kwenda Simba
kama inavyopotoshwa. KamaNgasa anataka kuvunja mkataba wake au kama
Yanga bado wanamhitaji basi waje na dola 50,000 na Azam FCitawauzia
kwani licha ya kwamba amepelekwa kwa mkopo simba lakini Ngasa bado ni
mali ya Azam FC
8. Tunaomba kuweka msimamo wetu kuwa hatupo
tayari kumlipa Ngasa na kuvunja mkataba wake na hatunasababu ya kufanya
hivyo. Kama Ngasa hataki kwenda tunakompeleka Azam FC inamruhusu kubakia
klabuni nakutumikia adhabu.
9. Lakini Ngasa na washauri wake
waelewe kuwa akiamua kubaki Azam FC atakaa nje ya uwanja kwa muda
woteuliosalia kwenye mkataba wake, kwani Azam FC haipotayari kumvisha
jezi mchezaji anayefanya vitendo vya utovu
wanidhamu.
Imetolewa na utawala.
Azam FC
Kutoka maktaba ya simba na yanga fans
About Omari Makoo
0 comments :
Post a Comment