-->

MTUHUMIWA VICTOR AMBROSE WA KESI YA KULIPUA KANISA AFIKISHWA KORTINI


Kijana mwenye umri upatao miaka 20 ambaye amefahamika kwa jina la Victor Mwambose mwendesha bodaboda ambae ni mtuhumiwa wa mlipuko uliotokea  kanisani katika mkoa wa Arusha amefikishwa kortini huku raia wanne wa nchi za Kiarabu wameachwa huru baada ya kuonekana kwamba hawakuhusika kabisa katika mlipuko huo.Raia hao wanne ambao hapo mwanzo ilisemekana kwamba ni wasaudia imetambulika kwamba si wote kwamba ni wasaudia bali ni mmoja tu ndio msaudia na wengine wanatoka falme za kiarabu na ni watu muhimu katika mataifa yao.
Victor Ambrose alifikishwa mahakamani hapo jana katika mahakama ya Hakimu Mkazi wa mkoa wa Arusha tayari kwa kusomewa mashtaka mawili ya kuuwa na kujaribu kuuwa mbele ya Hakimu Devotha Kamuzora.
Mtuhumiwa Victor Ambrose aliosomewa mashtaka mawili ya kuua na kujaribu kuua watu katika tarehe 5 ya mwezi wa 5 katika muda wa saa 4:30 na 5:00 asubuhi.Hata hivyo kesi hiyo ili ahirishwa hadi Mei 27.
Pia kulikuwa na watuhumiwa wengine ambao nao walikamatwa katika kipindi cha harakati za kuwatafuta wahusika ambao wameshiriki kwenye tukio hilo,Kamanda wa mkoa wa Arusha Liberatus Sabas alisema kwamba bado watuhumiwa hao wanahojiwa na polisi na maelezo bado hayajatosha kupelekwa mahakamani.Watuhumiwa hao ni Yusuph Lomayani'Josee'(18),George Silayo(23),Mohamed Said(38) na Jasm Mubarak.
MTUHUMIWA VICTOR AMBROSE

source:Gazeti la habari leo Mei 14,2013
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment