-->

MH ZITTO KABWE KUHAMIA CCM??


Hili ndio swali ambalo limekuwa likiumiza vichwa ikiwa zimebaki siku chache ili CHADEMA iweze kufanya maamuzi ya mwisho baada ya kuwapa wiki mbili wakina Dkt. Kitila,Mwigamba pamoja na Mh Zitto Kabwe ili kujibu shutuma zilizo mbele yao ambazo zimepelekea kunyang'anywa vyeo ndani ya chama hicho,Kikosi hiki cha watu wa tatu walionyang'anywa vyeo wamekuwa mhimili kwa muda mrefu sana katika chama hicho kwa kutumia akili pamoja na nguvu kwenye kukijenga chama hicho.Zitto Kabwe pamoja na kuwa ni mwanachama wa CHADEMA na pia alikuwa na nyazfa za uongozi katika chama hicho pia alikuwa akipendwa na wananchi pamoja na wanachama wa vyama vingine kama vile CUF,CCM,NCCR MAGEUZI pamoja TLP.
Zitto Kabwe amekuwa akitajwa kwamba ni kibaraka wa CCM na huku wengine wakiamini kuwa amepewa mapesa na CCM ya kukihujumu chama cha hicho cha CHADEMA.Mpaka sasa hakuna ushahidi uliothibitika dhidi ya tuhuma hiyo kwani hata ule ulioitwa WARAKA WA SIRI WA ZITTO KABWE umegundulika kuwa ni wakugushi na wala hauna ukweli.
Mwaka 2009 mchezaji wa Manchester united C.Ronaldo ambae alikuwa kipenzi cha Mashabiki wa Man U aliihima timu hiyo na kuhamia timu ya Real madrid,kitendo cha yeye C.Ronaldo kuhamia timu hiyo kilipelekea mashabiki wengi wa wa Manchester united kuishabikia timu hiyo ya Real madrid.Je kama Mh Zitto Kabwe atahamia CCM na wanachama wa CHADEMA watafuata mapenzi yao kwa kuhamia huko??
Kwa hakika bado ni kitendawili ila muda ndio utasema kweli
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment