Kampuni
ya Transevents Marketing Ltd ya Tanzania kwa kushirikiana na kampuni la
Dutch Amfibious Transport(DAT) linalotengeneza mabasi kutoka Uholanzi
yenye uwezo wa kutembea nchi kavu na majini na ambayo itakuwa ni
Teknolojia ya kwanza kwa Afrika itakayoanzia Tanzania.
Mabasi
hayo ya aina yake ambayo yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria wa kutosha
yanatarajiwa kuzinduliwa mwakani nchini Tanzania , pamoja na hayo mabasi
hayo yataweza kupunguza foleni kwa kiasi kikubwa na kurahisisha swala
zima la usafiri ambapo mabasi hayo na baadhi ya magari mengine madogo
yatakuwa na uwezo wa kupita majini na Nchi kavu.
Baadhi ya Mabasi hayo yatakuwa yanatokea Mombasa hadi Mtwara kupitia Baharini kisha nchi kavu. Mchakato
huu umekwisha anza kufanyiwa upembuzi yakinifu kwa ushirikiano na
taasisi pamoja na Mamlaka mbalimbali za hapa nchini zikiwemo, SUMATRA,
Jeshi la Polisi na kitengo cha Usalama barabarani.
Video hizi Mbili zinaelezea kwa kina na kuonesha jinsi Mabasi haya yatakavyokuwa yakifanya kazi hapa nchini Tanzania
Tazama Video za Basi hilo tangia Linatengenezwa hadi Linafanyiwa majaribio
0 comments :
Post a Comment