Donald Mosoti Omwanwa akisanini mkataba wa miaka miwili
Ivo Mapunda akisaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba mbele ya katibu mkuu wa timu hiyo Evodius Mtawala.
Mapunda amesema beki huyo wa kati ambaye amesaini kuichezea Simba siku moja kama ilivyokuwa kwake ni beki mzuri na wa uhakika.
“Ni wazo zuri, ninaamini Musoti atasaidia kwa kuwa ndiye alikuwa beki wetu tegemeo.
“Nafikiri hajacheza mechi chache sana za ligi tokea misimu miwili iliyopita,” alisema Ivo.
Musoti
na Ivo walikuwa wanakipiga pamoja na kikosi cha Gor Mahia ya Kenya
ambacho walifanikiwa kukipa ubingwa baada ya kuukosa kwa zaidi ya miaka
12.
Wote wawili wametua Simba na tayari wameishaanguka saini.
Wanatarajiwa kuanza kazi Msimbazi mara moja chini ya kocha mpya ‘Mheshimiwa’ Logarusic.
0 comments :
Post a Comment